Friday, April 5, 2019

IKULU YAKANUSHA TAARIFA INAYOSAMBAZWA KUHUSU CAG, BUNGE

  Malunde       Friday, April 5, 2019

Baada ya kusambaa kwa taarifa katika mitandao ya kijamii kwamba Rais amesikitishwa na kitendo cha Bunge la Tanzania kuazimia kutofanya  kazi na ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi wa Hesabu za Serikali, Ikulu imekanusha na kudai kwamba taarifa hizo hazina ukweli.

Mkurugenzi wa Mawasiliano Ikulu, Gerson Msigwa amesema kuwa Taarifa hizo zinazosambazwa hazina ukweli wowote na badala yake zinapaswa kupuuzwa.

Taarifa iliyokanushwa na Ikulu ilikuwa ikisema kwamba, "Ikulu inalikumbusha Bunge kwamba tayari CAG, amekwisha wasilisha ripoti yake kwa Rais hivyo inatakiwa kuja bungeni kama Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inavyoelekeza. Pia Bunge litambue Mammlaka ya CAG na  kwamba hawajibiki kwa Spika wala Bunge".

Taarifa hii ya kughushi imetoka siku chache baada ya April 2, 2019, Bunge la Tanzania kuazimia kutofanya kazi na Mdhibiti na Mkaguzi wa Hesabu za Serikali CAG, Prof Mussa Assad kwa kutoa kauli iliyoashiria kulidhalilisha Bunge baada ya kusema kuwa Bunge ni 'dhaifu'.Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post