Monday, April 8, 2019

MBOWE KUPANGUA BARAZA LAKE LA MAWAZIRI KIVULI BUNGENI

  Malunde       Monday, April 8, 2019

Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani bungeni, Freeman Mbowe amesema muda wowote kuanzia sasa atapangua Baraza la Mawaziri Vivuli na kuwaondoa wabunge wa CUF kutokana na baadhi yao kumuunga mkono Mwenyekiti wa CUF, Prof. Ibrahim Lipumba, na baadhi ya waliokuwa viongozi wa CUF kuhamia ACT Wazalendo.

Hata hivyo, CUF kupitia kwa Magdalena Sakaya  imesema ikitokea mabadiliko yoyote ya aina hiyo watamuandikia barua Spika kuomba ziwepo kambi mbili za upinzani bungeni, na hivyo stahiki za kambi ya upinzani zitakwenda katika makundi mawili.


“Lakini wakileta tatizo lolote sisi tuna haki, tutaandika barua kwa Spika kuwepo kambi mbili. Kwa hiyo stahiki za kambi za upinzani bungeni zitagawanywa mara mbili.” Amesema Sakaya

Sakaya alizitaja stahiki hizo kuwa ni mfuko kwa ajili ya wapinzani unaowawezesha kutekeleza mambo mbalimbali ikiwemo kuajiri watu wa kuwaandikia barua.

Akijibu hoja hiyo, Mbowe amesema wanaweza kufanya wanavyotaka, ikiwa kanuni na sheria zitawaruhusu na kusisitiza kuwa wao (CHADEMA) hawawezi kushirikiana na chama ambacho hakiko katika ushirikiano wao.

Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post