DC AKANUSHA UWEPO WA KIWANDA CHA KUTENGENEZA UUME BANDIA IRINGA


NA FREDY MGUNDA,IRINGA.
Siku chache baada ya kusambaa kwa picha zinazomuonesha Mkuu wa Wilaya ya Iringa Richard Kasesela akiwa ameshika viungo bandia vya kiume na kuzua Taharuki katika jamii, Mkuu huyo wa Wilaya ametolea ufafanuzi.

Akizungumza na Wandishi wa habari ofisini kwake leo Kasesela amesema kuwa taarifa zilizosambaa mtandaoni juu ya uzalishaji wa viungo bandia vya kiume, zimeleta changamoto huku akiwataka wananchi kuondokana na dhana potofu za kuchukua habari za mitandaoni na kuupotosha umma.

“Naomba niendee kuwaomba radhi watanzania kwa ajili ya jambo ambalo lilileta taharuki kwenye mitandao ya kijamii hasa nchi ya jirani zetu hapo Kenya lilipokelewa tofauti na nilivyokuwa hapo awali” alisema Kasesela

Kasesela aliwataka watanzania kuacha kufuatia mambo ya ajabu na kuyapa nafasi kwenye mitandao ya kijamii kuliko kupata mambo ya kujenga nchi na yenye tija.

“Jamni ile habari ilitungwa na ni habari ya hovyo sana kwa kuwa nililishwa habari ambayo mimi sijaisema kwenye chombo chochote kile kwenye vyombo vya habari hivyo hiyo habari ni ya kupuuza tu” alisema Kasesela

Kasesela amewashauri watanzania kuhakikisha wanafatilia taarifa zenye kuleta maendeleo na zenye kujenga katika jamii inayomzunguka.

“Kwa sasa habari nyingi ambazo zinazungumzwa hivi sasa ni habari ambazo ni za hovyo hovyo mno ndio maana leo wamesema kuwa wilaya ya Iringa kuna kiwanda hicho kitu ambacho sio kweli” alisema Kasesela

Katika hatua nyingine Mkuu wa Wilaya ya Iringa Richard Kasesela amelaani kitendo cha Dawson Kagine kusambaza taarifa zisizo za kweli na kuongeza kuwa mkoani Iringa kuna kiwanda cha kuzalisha vifaa vya elimu ya mapambano dhidi ya Ukimwi.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527