CHUO CHA UONGOZI WA MAHAKAMA LUSHOTO(IJA) CHAWANOA WADAU MBINU ZA KUENDESHA MASHAURI YA WATOTO


Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Kanda ya Arusha,Mosses Mzuna akifungua mafunzo ya wadau wa haki za Mtoto katika mikoa ya Arusha na Manyara jijini Arusha ,kushoto ni Mratibu wa mafunzo,Mwanabaraka Mnyukwa na Mkurugenzi wa Chuo Kikuu Huria kituo cha Arusha,Marcel Masalu. 
Afisa Ustawi wa Jamii Mahakama ya Watoto Kisutu,Asha Mbaruku akizungumza wakati wa mafunzo ya wadau haki za mtoto yaliyoandaliwa na Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto(IJA). 
Naibu Msajili Msajili wa Mahakama Kuu kanda ya Dar es Salaam,Nyigulila Mwaseba akizungumza wakati wa mafunzo ya siku tano ya wadau haki za mtoto yanayofanyika jijini Arusha. 
Hakimu Mkazi wa Mahakama ya wilaya Arusha ,Chrisanta Chitanda akizungumza wakati wa mafunzo hayo. 
Hakimu Mkazi wa Mahakama ya wilaya Arumeru,Benard Nganga(katikati),Hakimu Mkazi wa mahakama hiyo,Amelia Mushi(kushoto) na Hakimu Mkazi mahakama ya wilaya ya Arusha,Chrisanta Chitanda wakibadilishana mawazo wakati wa mapumziko .


Mwandishi Wetu,Arusha

Maafisa wa Mahakama wametakiwa kuwa makini katika kufatilia na kuendesha mashauri yanahusu watoto ili kulinda haki zao zinazotajwa katika mikataba ya kimataifa,katiba ya nchi na sheria mbalimbali.

Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu kanda ya Arusha,Mosses Mzuna amesema hayo wakati akifungua mafunzo ya siku tano kwa Mahakimu,Waendesha Mashtaka wa serikali,Mawakili wa kujitegemea na maafisa ustawi wa jamii yanayofanyika jijini hapa.

Alisema katika kuweka umuhimu wa kulinda haki za watoto serikali ilianzisha mahakama ya watoto iliyoanzishwa kupitia ibara ya 97 ,Sura ya 21 ya mwaka 2009 na mafunzo hayo yamekuja wakati muafaka ili kuwapa uwezo maafisa wanaohusika katika mashauri ya watoto.

Mratibu wa mafunzo ambaye ni Mkufunzi katika Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto(IJA) walioandaa mafunzo hayo kwa kushirikiana na Mahakama nchini,Mwanabaraka Mnyukwa alisema mafunzo hayo yanalenga kuwajengea uwezo maafisa hao kuendesha mashauri wakiwa na uelewa wa sheria ya mtoto.

“Mtoto ni sehemu muhimu katika jamii kutokana na uwezo wao wanashindwa kujitetea dhidi ya matukio mabaya wanayotendewa ndio maana ipo sheria inayowalinda lakini inapotokea wamefanyiwa mambo ambayo ni kinyume cha sheria zifuatwe taratibu zinazostahili kuwalinda watoto na kuwaadhibu watuhumiwa,”amesema Mnyukwa.

Alisema wadau hao wanajengewa uwezo baada ya shirika la kimataifa linahusu watoto(UNICEF) kufadhili mafunzo hayo katika kanda za kimahakama kwenye mikoa ya Mbeya,Mara,Tanga,Tabora,Mwanza ,Dar es Salaam na sasa Arusha.

Naibu Msajili wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu,Augustine Rwizile alisema Tanzania ikiwa mojawapo ya nchi nyingine duniani imeridhia mikataba ya kimataifa inayolinda haki za binadamu pamoja mtoto kwa ujumla.

Alisema licha ya changamoto ya watoto kushindwa kujieleza mahakamani kutokana na mazingira yalivyobado jamii na maafisa wanaohusika katika michakato ya mashauri hayo wanaowajibu wa kuhakikisha haki inatendeka. 

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post