BOBI WINE AANDAA MAANDAMANO UGANDA


Leo April 23, 2019 , msanii na mbunge, Bobi Wine anatarajia kuwasilisha rasmi barua Polisi kuwafahamisha kuhusu maandamano yake ya amani kupinga kuzuiwa  vyanzo vyake vya mapato.

Hatua ya Bobi Wine inafuatia polisi kuzuia tamasha lake kwa madai kwamba hawakuwa na uwezo kudhibiti maelfu ya mashabiki wake.

Jana Bobi Wine ambaye ni mbunge wa upinzani, alitiwa nguvuni kwa saa kadhaa baada ya kumkamata alipokuwa njiani kuelekea kwenye hoteli iliyoko iliyopo Ziwa Victoria ambako alikuwa akipanga kuzungumza na waandishi wa habari kuhusu  hatua ya Serikali kumzuia kufanya tamasha lake la Pasaka.

Rais Museveni anasema hatavumilia matamasha yanayochanganywa na siasa. Wine alisema Museveni anataka kuwazuia wanamuziki wote ambao hawamuungi mkono.

''Rais Museveni amewaagiza polisi kuzuia matamasha yangu kwa sababu hapendi kusikia ninachokiimba. Alitaka mimi niwe kama baadhi ya wasanii wanaoimba nyimbo za kumsifu na nilipokataa akaamua kuwa hataniruhusu kufanya onyesho lolote la muziki wangu nchini Uganda,’’ alisema.


Video ya kukamatwa kwake ilionyesha polisi wa kuabiliana na ghasia wakiingia kwa nguvu ndani ya gari lakekatika eneo la Busabala.

Bobi Wine alikamatwa na kuingizwa katika gari la polisi na kupelekwa eneo lisilojulikana.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527