WACHINA WATOA MSAADA WA BIA

Kampuni ya uchimbaji madini ya Ghuanshan International inayomilikiwa na Wachina nchini Kenya, imezua mtafaruku baada ya kupeleka msaada wa bia eneo la Tiaty, ambao wamekumbwa na balaa la njaa.

Mnamo Ijumaa, Aprili 5, kiwanda cha kuchimba madini cha Ghuanshan International Mining Company Limited, kilifunga safari na kuelekea Kaunti ya Baringo na malori yaliyojaa mazuri ambayo yangeleta tabasamu miongoni mwa wakaazi wa eneo la Tiaty. 


Malori hayo yaliwasili yakiwa yamebeba chakula cha msaada kwa waathiriwa wa baa la njaa, ikiwemo katoni 20 za mvinyo kila moja ikiwa na mikebe 24. 
Kampuni hiyo ambayo iliamua kuunga mkono jitihada za kunusuru jamii zilizokumbwa na uhaba wa chakula kutokana na ukame, kwa kwenda kuwapa msaada wa vyakula mbali mbali zikiwemo na bia, jambo ambalo limeleta mtafaruku mkubwa nchini Kenya.

Wakati msaada huo ukitolewa katika eneo la shule ya Katikit iliyopo Tiaty, wazee na watoto walikuwa wakitazama, huku vijana wakigombania misaada hiyo.
Mkurugenzi wa kampuni hiyo Khan Ke amesema kwamba waliamua kuweka na bia kwenye vyakula walivyowapelekea, baada ya kugundua kuwa wakazi hao pia wanapenda bia/mvinyo.

Hata hivyo wataalamu wa afya waliingilia kati wakisema kuwa jambo hilo sio sahihi, akiwemo Mkurugenzi wa Afya nchini humo Dkt. Kepha Ombacho, ambaye amesema si sawa kiafya kupeka bia kwatu ambao wana njaa, kwani tumbo lisilo na kitu likikutana na pombe hufanya kazi kwa haraka sana na mwishowe huleta madhara.

Wakati wa kutoa msaada huo, kulizuka vuta nikuvute baina ya wenyeji ambao kila mmoja alitaka kujinyakulia kipande kikubwa zaidi ya wenzake -Kanisa la SDA hata hivyo limelaumu hatua hiyo na kusema kuwa wangewapa wakaazi maji na maziwa badala yake.

  Katika ripoti ya Edaily, Jumamosi, Aprili 6, kanisa la Seventh Day Adventist (SDA), kupitia kwa mkutano wa Bonde la Kati uliotoa chakula cha msaada katika eneo hilo, walilaani vikali hatua ya kampuni hiyo kuwapa mvinyo wakaazi. 

Wakiongozwa na Anita Too, ambaye ni kiongozi wa wanawake wa dhehebu hilo, kanisa hiyo ilisema kuwa, ni vyema kampuni hiyo ingewapa waathiriwa maziwa na maji.

 Too alipendekeza kuwa, kampuni hiyo ingechimba visima ili visaidie katika kuzalisha maji ambayo yangewafaa wakazi katika matumizi yao ya kila siku, na kunyunyiza mashamba yao katika ukulima. 

 Muungano huo wa kanisa la SDA, ulitoa magunia mia mbili ya 90kg ya mahindi, magunia 200 ya 50kg ya mchele, magunia kumi ya 90kg ya maharagwe na magunia kumi na sita ya 2kg ya unga wa sima. Bidhaa hizo ziliwafaidi takriban wakaazi 500 wa eneo la Nginyang. 

Kando na kiwanda cha Ghuanshan kuwapa wakaazi pombe, kilitoa magunia 300 ya mahindi na mitungi 20 ya mafuta ya kupika, bidhaa ambazo zilisambazwa kwa njia ya vurugu. 

Hata hivyo wakazi wa maeneo hayo wameonekana kufurahia misaada hiyo ikiwemo pombe, kwani walionekana wakigombania na wengine kukimbia nazo kwenda kuhifadhi nyumbani.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post