Monday, March 25, 2019

ZITTO KABWE AFUNGUKA FURAHA YA AFCON TZ, JPM KUVAA NGUO KAMA YA ACT WAZALENDO

  Malunde       Monday, March 25, 2019

Zitto Kabwe akiwa na Rais Magufuli pichani.

Kiongozi wa Chama cha ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe, amefunguka kuwa ushindi wa Taifa stars jana dhidi ya timu ya taifa ya Uganda 'The Cranes' umeliunganisha taifa pasi na kujali itikadi za vyama.

Zitto kupitia ukurasa wake wa Twitter ameandika kuwa, ''mpira umeleta muunganiko kwa taifa na kuleta furaha nchini, huku akifurahishwa na shati alilokuwa amevaa Rais Magufuli lenye rangi ya zambarau ambayo ni rangi inayotumiwa na chama chake.

"Nguvu ya mpira kuunganisha nchi ni ya aina yake. Kina Samatta kuwezesha Tanzania kufuzu ‘Mataifa Huru Afrika’ #AFCON nchi iliyokuwa imenuna, imejawa furaha. Hata Rais kuonyesha Umoja alivaa shati la Zambarau, rangi ya Chama Cha ACT-Wazalendo akitazama mechi Ikulu", ameandika Makonda.

Taifa Stars imeungana na timu ya taifa ya Uganda, Kenya na Burundi zitakazoiwakilisha Afrika Mashariki katika michuano ya AFCON itakayofanyika kuanzia mwezi June hadi Julai, 2019 nchini Misri.
Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post