Picha : PAWWCO,IDARA YA MAENDELEO YA JAMII WATOA MSAADA KWA WAZEE USANDA KUADHIMISHA SIKU YA WANAWAKE DUNIANI


Idara ya Maendeleo ya Jamii halmashauri ya wilaya ya Shinyanga kwa kushirikiana na Shirika la PAWWCO linalojishughulisha na shughuli za kijamii mjini Shinyanga, wametembelea kambi ya kulea wazee kwenye kituo cha Usanda na kutoa msaada wa nguo, sabuni za kufulia pamoja na chumvi, katika kuelekea kuadhimisha siku ya wanawake duniani hapo kesho.


Zoezi la utoaji wa msaada kwa wazee hao limefanyika leo Machi,7,2019 likiongozwa na Mkuu wa Idara ya Maendeleo ya Jamii wa halmashauri ya wilaya ya Shinyanga Deusi Mhoja.

Akizungumza kabla ya kukabidhi msaada huo,Mhoja amesema wazee hao ni hazina ya taifa hivyo wanapaswa kuhudumiwa na kutunzwa kwani ndiyo waliopigania taifa hili katika kupata uhuru, ambapo kwa sasa hawana nguvu tena na kilichobaki ni kazi ya jamii kuwahudumia ikiwa ni pamoja na kuwapatia chakula.

“Katika kuelekea kilele cha maadhimisho ya siku ya wanawake duniani Machi 8, sisi kama halmashauri kwa kushirikiana na wadau wetu wa maendeleo Shirika la PAWWCO, tumeona ni jambo la muhimu kuwakumbuka bibi zetu hawa kwa kuwapatia msaada wa nguo, chumvi pamoja na sabuni za kufulia,”amesema Mhoja.

Naye mratibu wa Shirika la (PAWWCO) Madaga Joseph, amesema Shirika hilo litaendelea kushirikiana na Serikali katika kutatua changamoto mbalimbali ndani ya jamii, ikiwamo na kambi hiyo ya kulea wazee.

Kwa upande wao wazee hao akiwemo Elizabeth Mhari, wameshukuru kupatiwa msaada huo, huku wakiomba kutatuliwa changamoto mbalimbali ambazo zinawakabili kwenye kambi hiyo, ikiwemo na utengenezaji wa choo ambapo kilichopo ni kibovu na kimeshajaa hali ambayo wanahofia usalama wa afya zao.


TAZAMA MATUKIO KATIKA PICHA HAPA CHINI

Mkuu wa Idara ya Maendeleo ya Jamii halmashauri ya wilaya ya Shinyanga Deus Mhoja akizungumza kwenye kambi ya wazee Usanda na kusema  Serikali ipo nao bega kwa bega katika kutatua changamoto zinazowakabili kwa kushirikiana na wadau wa maendeleo. Picha zote na Marco Maduhu - Malunde1 blog

Mkuu wa idara ya maendeleo ya jamii halmashauri ya wilaya ya Shinyanga Deus Mhoja akigawa sabuni kwa wazee.Mratibu wa miradi kutoka Shirika la PAWWCO Madaga Joseph akitoa msaada wa nguo kwa wazee.Zawadi zikiendelea kutolewa.

Afisa Maendeleo ya Jamii halmashauri ya wilaya ya Shinyanga Aisha Omari akisalimia na wazee hao huku utoaji wa msaada ukiendelea.

Msaada ukiendelea kutolewa.

Afisa Maendeleo ya Jamii halmashauri ya wilaya ya Shinyanga Aisha Omari akitoa msaada wa nguo kwa wazee hao kambi ya Usanda.

Utoaji wa msaada ukiendelea.

Wazee wakiendelea kupokea zawadi.Wazee wakiwa na zawadi zao.

Mzee Elizabeth Mhali akishukuru kwa msaada wa vitu hivyo ambayo wamepewa na Idara ya maendeleo ya jamii pamoja na Shirika la PAWWCO, na kuomba watatuliwe changamoto ya ubovu wa choo ikiwa kilichopo kimeshajaa na kuhofia usalama wa afya zao.

Mzee Zacharia Makaranga, akiomba wadau wajitokeze kuwasaidia msaada wa chakula.

Awali wazee wakisalimiana na viongozi kutoka Idara ya maendeleo ya jamii ya halmashauri ya wilaya ya Shinyanga mara baada ya kuwasili kambini hapo kutoa msaada wa nguo, chumvi pamoja na sabuni za kufulia.

Wazee wakipiga picha ya pamoja na viongozi wa idara ya maendeleo ya jamii halmashauri ya wilaya ya Shinyanga na Shirika la PAWWCO  baada ya kumaliza kupokea misaada mbalimbali katika kuelekea siku ya maadhimisho ya wanawake duniani.

Na Marco Maduhu- Malunde 1 Blog

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post