WASOMI NCHINI WATAKIWA KUWEKEZA KATIKA TAFITI


Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Dk. Leonard Akwilapo, akizungumza wakati wa ufunguzi wa kongamano la Kimataifa la kwanza katika Chuo Cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere Kampasi ya Kivukoni
Mkuu wa Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere (MNMA), Profesa. Shadrack Mwakalila akitoa neno kwa wana taaluma waliohudhulia katika Kongamano la Kimataifa 
Naibu Mkuu wa Chuo Taaluma Prof. Richard Kangalawe akitoa Salamu za Ukaribisho kwa Wanataaluma waliohudhuria katika Kongamano la kwanza la kimataifa 
Naibu Mkuu wa Chuo - Utawala Dk. Godwin Kaganda akitoa neno la shukrani kwa wana Taaluma waliofika katika kongamano hilo.
Balozi wa Urusi nchini Tanzania, Mh Yuri Popov akisalimia Washiriki waliofika katika Kongamano la Kimataifa lililoandaliwa na Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere kwa kushirikiana na Chuo cha Sayansi ya Jamii kwa Afrika kutoka Urusi. 
Baadhi ya wageni walioshiriki kwenye kongamano hilo lenye kauli mbiu ya 'State Building in Africa: Prospects and Challenges’.
Baadhi ya wageni walioshiriki kwenye kongamano hilo lenye kauli mbiu ya 'State Building in Africa: Prospects and Challenges’. Zaidi ya nchi saba zimeshiriki katika Kongamano hilo.
Baadhi ya wageni walioshiriki kwenye kongamano hilo lenye kauli mbiu ya 'State Building in Africa: Prospects and Challenges’ 
Viongozi wa Meza Kuu wakiwa katika Picha ya Pamoja na baadhi ya Wadau na wana taaluma kutoka Mataifa mbalimbali walioshiriki Kongamano la Kimataifa katika Chuo cha Kumbukumbu ya MwalimuNyerere Kampasi ya Kivukoni
**
 Na Humphrey Shao,Globu ya Jamii

Wasomi Vyuo Vikuu na vyuo vya elimu ya juu nchini wametakiwa kuwekeza katika tafiti mbalimbali ili kuweza kuisadia Jamii ya kitanzania katika harakati za kufikia uchumi wa kati.

Hayo yamesemwa leo na Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia Dk. Leonard Akwilapo alipokuwa kifungua kongamano la siku tatu la kimataifa la lenye kauli mbiu ya ‘State Building in Africa: Prospects and Challenges’ lililofanyika katika Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere kampasi ya Kivukoni Dar es Salaam.

“Tafiti zinatija kubwa katika maendeleo ya jamii kwa sababu wasomi hutambua majibu sahihi ambayo hutoa dira ya kuisaidia jamii. Vyuo vinamajukumu matatu, kufundisha , kutafiti na kuhudumia jamii, kwa hiyo elimu inayotolewa na vyuo inatakiwa kurudisha huduma kwa jamii kwa kuwa na majibu sahihi ya kusaidia maendeleo ya watu,” anasema Akwilapo.

Kwa upande mwingine Mkuu wa Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere (MNMA), Profesa. Shadrack Mwakalila alisema kongamano hilo la Kimataifa limewakutanisha wanazuoni kutoka mataifa mbalimbali.

Anasema kusudio la kongamano hilo ni wanazuoni kuchakata mawazo kwa kuchambua tafiti mbalimbali kwa lengo la kujenga nchi za Kiafrika.

“Kongamano hili la Kimataifa ni la kwanza kufanyika hapa Chuoni. Ila Chuo kina utamaduni wa kufanya makongamano mara kwa mara kwa lengo la kukutanisha wasomi na wadau wa elimu na maendeleo kujadili mambo mengi yanayotokana na tafiti walizozifanya ikiwa ni pamoja na Kukumbuka Waasisi wa Taifa letu.” anasema Profesa Mwakalila.

Kwa upande wake Naibu Mkurugenzi wa Utafiti wa Chuo cha Sayansi ya Jamii kwa Afrika kutoka Urusi, Dk. Dmitri M. Bondarenko alisema Chuo chao kimejikita katika tafiti za kutafuta suluhu ya changamoto zinazoikabiri jamii.

“Kujenga Taifa baada ya uhuru ilikuwa rahisi lakini changamoto za sasa kutokana na utandawazi zinachochea kupoteza uzalendo hatua ambayo imesababisha changamoto kubwa kwa nchi nyingi kupiga hatua za kimaendeleo,” anasema Dk. Bondarenko.

Awali akitoa salam za ukaribisho, Naibu Mkuu wa Chuo – Taaluma Prof. Richard Kangalawe amesema Kongamanao hilo limeandaliwa na Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere kwa kushirikiana na Chuo cha Sayansi ya Jamii kwa Afrika kutoka Urusi.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post