Tazama Picha : MATUKIO MBALIMBALI KWENYE MSIBA WA RUGE MUTAHABA BUKOBA | MALUNDE 1 BLOG

Monday, March 4, 2019

Tazama Picha : MATUKIO MBALIMBALI KWENYE MSIBA WA RUGE MUTAHABA BUKOBA

  Malunde       Monday, March 4, 2019
Mazishi ya aliyekuwa Mkurugenzi wa vipindi na uzalishaji wa Clouds, Ruge Mutahaba yamehudhuriwa na vigogo zaidi ya kumi wakiwemo Mawaziri, Wabunge na Wakuu wa Mikoa.Ratiba iliyotolewa leo asubuhi Jumatatu Februari 4,2019 inawataja baadhi ya vigogo hao ambao ni mawaziri na wizara zao kwenye mabano ni Dk Hamisi Kigwangalla (Maliasili na Utalii), Dotto Biteko (Madini), January Makamba (Muungano mazingira), Angela Kairuki(uwekezaji) na Juma Aweso ambaye ni Naibu Waziri wa Maji.

Pia, wabunge wanaotajwa kwenye ratiba hiyo ni Nape Nnauye (Mtama-CCM), Rudhiwani Kikwete (Chalinze-CCM), Aieshi Hilary (Sumbawanga Mjini- CCM) na wabunge wote wa Mkoa wa Kagera na wakuu wa wilaya.Wengine ni Wakuu wa mikoa ya Simiyu (Anthony Mtaka), Mwanza (John Mongella), Mara (Adam Malima) na Mkuu wa Wilaya ya Kakonko, Kanali Hoseah Ndagala.
Sanduku lenye mwili wa aliyekuwa Mkurugenzi wa Vipindi na Uzalishaji Clouds Media Group,Marehemu Ruge Mutahaba ukiwa tayari umewekwa katika uwanja wa Gymkana,Bukoba mkoani Kagera kwa ajili ya kuagwa,Ibada na baadae kurejeshwa tena Kiziru kwa ajili ya Mazishi.Katika sughuli hiyo viongozi mbalimbali wa Serikali,ndugu jamaa na marafiki wamefika uwanjani hapo kumpa heshima ya mwisho mpendwa wao.
Sanduku lenye mwili wa aliyekuwa Mkurugenzi wa Vipindi na Uzalishaji Clouds Media Group,Marehemu Ruge Mutahaba ukiwa tayari umewasili katika uwanja wa Gymkana,Bukoba mkoani Kagera tayari kwa kupewa heshima ya mwisho.


Waziri wa Madini, Mhe. Dotto Biteko akiwasili katika viwanja vya Gymkhana mjini Bukoba asubuhi hii katika ibada ya kumuaga aliyekuwa mkurugenzi wa vipindi Clouds Media Group marehemu Ruge Mutahaba.
Mkuu wa Mkoa Mara, Mhe. Adam Malima akiwasili kwenye viwanja vya Gymkhana mjini Bukoba asubuhi ya leo kuhudhuria ibada ya mazishi ya aliyekuwa mkurugenzi wa vipindi Clouds Media Group marehemu Ruge Mutahaba inayofanyika viwanja vya Gymkhana mjini Bukoba. 
Hali ilivyo katika viwanja vya Gymkhana ndani ya manispaa ya Bukoba, ambapo viongozi mbalimbali, wananchi na wasanii wamejitokeza kumuaga aliyekuwa mkurugenzi wa vipindi Clouds Media Group marehemu Ruge Mutahaba.
Mbunge wa jimbo la Nyamagana, mkoani Mwanza Mhe. Stanslaus Mabula akimpa pole mkurugenzi wa Clouds Media Group Joseph Kusaga katika viwanja vya Gymkhana mjini Bukoba asubuhi hii katika ibada ya kumuaga aliyekuwa mkurugenzi wa vipindi Clouds Media Group marehemu Ruge Mutahaba. 
Mbunge wa jimbo la Nyamagana, mkoani Mwanza Mhe. Stanslaus Mabula akisalimiana na mbunge wa Kigoma mjini Mhe. Zitto Kabwe baada ya kuwasili katika viwanja vya Gymkhana mjini Bukoba asubuhi hii kumuaga aliyekuwa mkurugenzi wa vipindi Clouds Media Group marehemu Ruge Mutahaba. 
Mbunge wa jimbo la Sumbawanga mjini, Mhe. Aeshi Hillary akisalimiana na mbunge wa jimbo la Kigoma mjini, Mhe Zitto Kabwe katika viwanja vya Gymkhana mjini Bukoba asubuhi hii katika ibada ya kumuaga aliyekuwa mkurugenzi wa vipindi Clouds Media Group marehemu Ruge Mutahaba. 
Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post