WANAWAKE CHUO KIKUU ARDHI WAADHIMISHA SIKU YA WANAWAKE KWA KUTOA MSAADA KWA WATOTO WENYE SARATANI | MALUNDE 1 BLOG

Sunday, March 10, 2019

WANAWAKE CHUO KIKUU ARDHI WAADHIMISHA SIKU YA WANAWAKE KWA KUTOA MSAADA KWA WATOTO WENYE SARATANI

  Malunde       Sunday, March 10, 2019
Baadhi ya Wanawake wa Tawi la Chama cha wafanyakazi wa Elimu ya juu wa Chuo Kikuu Ardhi (ARU) wakiwa wamebeba dawa na mahitaji muhimu ya kibinadamu walipowasili katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) kutoa msaada kwa watoto wenye saratani jijini Dar es Salaam Machi 9 2019. (Picha zote na Robert Okanda)
Mwenyekiti wa Kamati ya Wanawake wa Tawi la Chama cha wafanyakazi wa Elimu ya juu wa Chuo Kikuu Ardhi (ARU), Dkt. Kerbina Moyo (wa pili kushoto) na Mhazini Grace Nakoba (kushoto) wakimkabidhi Peter Massawe, Mwakilishi wa wagonjwa wanaotibiwa kwenye wodi ya watoto wenye saratani katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH), sehemu ya msaada wa dawa na mahitaji muhimu ya kibinadamu jijini Dar es Salaam Machi 9 2019. Pamoja nao (wa pili kulia) ni Kaimu Msimamizi mkuu wa Wodi hiyo, Ephraim Kiswaga.
Sehemu ya Wanawake wa Chuo Kikuu Ardhi (ARU) wakishiki maandamano katika siku ya maadhimisho ya siku ya wanawake duniani. Maandamano yalianzia Chuoni hapo na kuhitimishwa eneo la Mlimani City jijini Dar es Salaam. 
Sehemu ya Wanawake wa Chuo Kikuu Ardhi (ARU) wakishiki maandamano katika siku ya maadhimisho ya siku ya wanawake duniani. Maandamano yalianzia Chuoni hapo na kumalizikia eneo la Mlimani City jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya Wanawake wa Tawi la Chama cha wafanyakazi wa Elimu ya juu wa Chuo Kikuu Ardhi (ARU) wakiwa wakipita mbele ya jukwaa wakati wa maadhimisho ya siku ya wanawake duniani yaliyohitimishwa katika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam hivi karibuni. Kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni Mhe. Sarah Msafiri na viongozi mbalimbali. 
Sehemu ya Wanawake wa Chuo Kikuu Ardhi (ARU) wakifuatilia matukio mbalimbali katika ukumbi wa Mlimani City wakati wa maadhimisho hayo jijini Dar es Salaam.Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post