BINTI AJINYONGA BAADA YA UGOMVI WA CHAPATI

Binti wa miaka 20, ajulikanaye kama Sharon, mkazi wa Kisumu, Kenya, amejinyonga hadi kufa baada ya majibizano baina yake na shangazi yake kuhusu chapati.

Inaelezwa kuwa Sharon aliachiwa fedha kwa ajili ya kununua chakula na kupika kwa ajili ya familia na badala yake alinunua chapati cha maharage na kula mwenyewe.

Kwa mujibu wa jirani wa familia hiyo, Jane Auma, shangazi yake aliporudi nyumbani na kuuliza kwanini binti huyo hakupika chakula cha familia nzima na badalayake akajinunulia chapati, wawili hao walianza kujibiza na baadaye, msichana huyo aliamua kujiua kwa kujinyonga.

Auma anasema ni ngumu kuamini kuwa msichana huyo angeweza kujinyonga kwa mzozo wa chapati, lakini hatahivyo ujumbe wa alioacha ameuandika tayari umefikishwa polisi.

Mwili wa marehemu umeshapelekwa kuhifadhiwa kwenye hospitali ya Jaramogi Oginga na upelelezi unaendelea. 

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527