SHIRECU YAFANYA MKUTANO MKUU, VIONGOZI WAANIKA MIKAKATI KABAMBE KUIPANGA UPYA SHIRECU


Chama Kikuu cha Ushirika mkoa wa Shinyanga (SHIRECU) kinakusudia kuanzisha Saccos ili kuwawezesha wakulima kukopa fedha ndani ya ushirika na kuwaepusha na changamoto ya kwenda kukopa kwenye taasisi
 za fedha na kutozwa riba kubwa,hivyo kuwa changamoto katika kupiga hatua ya maendeleo na kujikwamua kiuchumi.

Akizungumza kwenye mkutano mkuu wa 24 wa SHIRECU ambao umefanyika leo Machi 8,2019 katika ukumbi wa CCM mjini Shinyanga mwenyekiti wa SHIRECU mkoani Shinyanga Luhende Richard,amesema mbali na kuanzisha Saccos hiyo pia wameweka mkakati wa kuanzisha kituo cha cha Matangazo Redio ya SHIRECU ambayo itatumika kutoa elimu kwa wakulima juu ya kilimo bora na masoko.

Luhende amesema wameanza kuipanga upya SHIRECU ili
kuhakikisha wanatoa huduma zilizo bora kwa wakulima kutokana na hapo awali kukabiliwa na changamoto kubwa ya madeni ambayo aliyataja kuwa ni deni la umeme Tanesco shiling milioni 147, deni la TIB bilioni 14, kodi ya ardhi shilingi milioni 265 ambapo ameiomba wizara ya ardhi kuwaangalia kwa jicho la huruma kwani majengo mengi kwa sasa ni magofu.

“Mpaka sasa SHIRECU ina watumishi 126 ambapo zaidi ya 75 kati yao wamekaribia kustaafu na wengine muda wa kustaafu umefika lakini wanalazimika kuendelea na kazi kwani bado wanadai madai yao SHIRECU,tunaendelea na utaratibu wa kulipa mishahara na madai yao mengine,ambapo wakati bodi mpya ya Shirecu inaanza kazi Mei mwaka huu imekuta watumishi hawajalipwa mishahara yao miaka mitatu sawa na miezi 36 tayari tumeanza kulipa kadri fedha zinapopatikana”,amesema Luhende.

Amengeza kuwa walitembelea kanda zote saba za Shirecu ili kujionea mali za ushirika huo na kuweka mfumo ambao utasaidia kudhibiti upotevu wa mapato pamoja na kuzirejesha mali zilizokuwa zimechukuliwa na baadhi ya watu yakiwemo majengo, viwanja na mashamba na kusababisha ushirika huo kuyumba na kuingia kwenye madeni makubwa.

Akizungumza na wanachama wa SHIRECU kwenye mkutano huo mwenyekiti wa tume ya maendeleo ya ushirika nchini Dkt.Titus Kamani,amesema ushirika ulikuwa umegeuzwa kuwa kama shamba la bibi kutokana na baadhi ya watu
kutumia mali za SHIRECU na kuiacha haina kitu jambo ambalo amewatahadharisha viongozi kujiepusha na ubadhirifu wa mali za ushirika.

Amesema serikali imeamua kuhakikisha inasimamia ushirika ili uweze kuwa imara na kumsaidia mkulima na kutaka kuhakikisha viongozi wa SHIRECU wanasimamia kikamilifu umoja huo ili uweze kuleta tija.

Dkt. Kamani ametumia fursa ya mkutano huo kuweka jiwe la msingi kwenye ujenzi wa uzio wa shule hiyo na kukagua nyumba na magari ya SHIRECU yaliyofanyiwa ukarabati ili yaweze kuendelea kufanya kazi.
Mwenyekiti wa SHIRECU mkoa wa Shinyanga Luhende Richard Luhende akizungumza na wajumbe wa mkutano mkuu wa 24 wa SHIRECU.Alitumia fursa hiyo kueleza changamoto mbalimbali zilizopo na hatua walizochukuwa kukabiliana nazo tangu walivyochaguliwa Mei mwaka jana kushika wadhifa huo.
Wajumbe wa mkutano mkuu wa 24 wa chama cha Ushirika mkoa wa Shinyanga (SHIRECU) wakiwa  kwenye mkutano huo ambao umefanyika leo katika ukumbi wa CCM mjini Shinyanga. Katika mkutano huo wajumbe wamejadili mambo mbalimbali ya kujenga ushirika ikiwa ni pamoja na kuhakikisha wanawasimamia vizuri wakulima ili waweze kuuza pamba iliyo safi ili kuongeza thamani.
Wajumbe wakiendelea kufuatilia mkutano wa SHIRECU ukiendelea.
Mkutano unaendelea.
Mwenyekiti wa tume ya maendeleo ya ushirika nchini Dkt.Titus Kamani akiweka jiwe la msingi kwenye ujenzi wa uzio wa shule ya sekondari Buluba iliyopo manispaa ya Shinyanga,shule ambayo inasimamiwa na chama kikuu cha ushirika mkoa wa Shinyanga SHIRECU.
Kaimu mkuu wa shule ya sekondari Buluba Frednarnd Chuwa akisoma taarifa ya shule hiyo ,ambapo alisema shule ya Buluba inakabiliwa na tatizo la uchakavu wa miundombinu yake pamoja na kutokuwa na uzio ambao tayari umeanza kujengwa ili kuwaweka wanafunzi katika mazingira yenye usalama mzuri tofauti na ilivyosasa kila sehemu ni njia watu wanapita.
Baadhi ya wanafunzi wa shule ya sekondari Buluba wakiwa katika eneo lilipowekwa jiwe la msingi la ujenzi wa uzio wa shule hiyo.
Baadhi ya magari ya SHIRECU ambayo yamefanyiwa ukarabati tayari kwa ajili ya kuanza kazi ya kusaidia wanachama wake.
Wajumbe na baadhi ya viongozi wakitoka kukagua nyumba ya SHIRECU ambayo imefanyiwa ukarabati ili kuiweka katika hali nzuri. 

Picha zote na mwandishi wa Malunde 1 Blog.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527