MSANII BARNABA AANGUKA AKIMUAGA RUGE MUTAHABA


Msanii wa kizazi kipya Barnaba amesababisha vilio kutawala baada ya kushindwa kumalizia hotuba yake huku akiomba afunguliwe jeneza kumuona baba yake mlezi, Ruge Mutahaba.

Msanii huyo kutoka THT aliondolewa ukumbini akiwa amebebwa baada ya kuishiwa nguvu kutokana na uchungu mkali alio nao.

Alisema Ruge alikuwa kama baba kwake na hajawahi kumtoza mtu kati ya wasanii waliopita THT.

“Kama shida ni figo ungeniambia nikupe yangu, wazazi wangu walifariki Ruge ndiyo alikuwa Baba na ndio mama, Watoto wengi unawaoona THT wametoka kwenye maisha ya shida, Ruge alikuwa ndio Baba yetu” Alisema.Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post