CHINA YATANGAZA KUSITISHA SAFARI ZA NDEGE ZAKE ZENYE CHAPA YA BOEING 737 MAX 8

Kufuatia ajali ya ndege aina ya Boeing 737 ya Shirika la Ndege la Ethiopia iliyokuwa ikitoka Addis Ababa kwenda Nairobi na kuua watu 157, Mamlaka ya Udhibiti wa Safiri za Anga ya nchini China imetangaza maamuzi magumu.

Mamlaka hiyo imesema mapema Jumatatu, Februari 11 kuwa imeliagiza Shirika la Ndege la China kusitisha matumizi ya ndege za Boeing 737 hadi hapo itakapotoa taarifa zaidi kuhusu kurejea kwa safari zake.

Ndege ya Shirika la Ndege la Ethiopia aina ya 737 MAX 8 ilipata ajali dakika chache baada ya kuruka katika Uwanja wa Ndege wa Addis Ababa Jumapili, March 10.


Hiyo ni ajali ya pili ya ndege hizo ambazo ni toleo jipya la kampuni ya Boeing lililotolewa mwaka 2017, ambapo mnamo Oktoba mwaka 2018, ndege ya Shirika la Ndege la Indonesia iliyokuwa ikifanya safari za ndani ilianguka dakika 13 baada ya kuruka kutoka Uwanja wa Ndege wa Jarkata na kuua abiria 189 pamoja na wahudumu wa ndege.


Shirika la Ndege la China linamiliki jumla ya ndege 96 aina ya Boeng 737 MAX, ambapo imesema imeona mfululizo wa vyanzo vya ajali za ndege hizo zinafanana.


Lakini msemaji wa Shirika la Ndege la Boeing ameuambia mtandao wa Reuters akikanusha tuhuma hizo za China, akisema kuwa hana uhakika na taarifa ambazo nchi hiyo inazitumia.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post