ORODHA YA MIJI YENYE GHARAMA KUBWA DUNIANI NA MIJI YENYE GHARAMA YA CHINI

Paris ndio mji ulio na gharama kubwa zaidi duniani, ukiandamana na Hong Kong na Singapore.

Ni mara ya kwanza miji mitatu imekuwa katika nafasi sawa juu katika historia ya miaka 30 ya utafiti wa kila mwaka wa uchumi - Economist Intelligence Unit, inayolinganisha gharama katika miji 133 duniani.

Mji mkuu wa Ufaransa - ulio katika nafasi ya pili kwa gharam kubwa ya maisha mwaka jana - ndio nchi ya pekee ya Ulaya iliopo katika nafasi ya juu mwaka huu.

Utafiti huo umelinganisha bei za bidhaa za kawaida kama mkate katika miji 133.

Alafu inafuatilia iwapo bei hizo zimepanda au zimeshuka kwa kuzilinganisha na gharama ya maisha katika mji wa New York, Marekani.

Mithilisho

Mhariri wa ripoti hiyo Roxana Slavcheva amesema Paris umekuwa mojwapo ya miji kumi iliyo na gharama kubwa kuishi tangu 2003.

"Ni pombe tu, usafiri na tumbaku ulio na gharama nafuu ikilinganihswa na mataifa mengine ya Ulaya," amesema.

Kiwango cha gharama kwa mwanamke kukatwa nywele, kwa mfano inagharimu $119.04 mjini Paris, $73.97 mjini Zurich na $53.46 mjini Osaka nchini Japan.

Miji 10 yenye gharama kubwa duniani

1. Singapore (Singapore)

1. Paris (Ufaransa)

1. Hong Kong (China)

4. Zurich (Uswizi)

5. Geneva (uswizi)

5. Osaka (Japan)

7. Seoul (Korea Kusini)

7. Copenhagen (Denmark)

7. New York(Marekani)

10. Tel Aviv (Israeli)

10. Los Angeles (Marekani)

Mfumko wa bei na kutetelekea kwa sarafu kumesaidia msukumo wa mageuzi katika orodha ya mwaka huu huku matiafa kama Argentina, Brazil, Uturuki na Venezuela zikishuhudia kupungua kwa ukubwa gharama ya maisha .

Caracas huko Venezuela, ambako mfumko wa bei ulikaribia 1,000,000% mwaka jana na kuilazimu serikali kuidhinihsa sarafu mpya, ulioorodheshwa mji wenye gharama ndogo zaidi duniani mwaka huu.

Damascus nchini Syria iliorodheshwa mji wa pili wenye gharama ndogo zaiid duniani.

Utafiti huo wa Economist Intelligence Unit umeeleza kwamba "baadhi ya maeneo" gharama ya kuishi inapungua kutokana na athari za mtikisiko wa kisiasa au kiuchumi.

Miji 10 yenye gharama ya chini duniani

1. Caracas (Venezuela)

2. Damascus (Syria)

3. Tashkent (Uzbekistan)

4. Almaty (Kazakhstan)

5. Bangalore (India)

6. Karachi (Pakistan)

6. Lagos (Nigeria)

7. Buenos Aires (Argentina)

7. Chennai (India)

8. New Delhi (India)

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527