MICHEPUKO MINGI CHANZO CHA KUZALIWA WATOTO WENGI WA KIKE


Ofisa Programu ya Uzazi Salama kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Martha Shakinyau, amesema moja ya sababu za kuzaliwa kwa watoto wa kike wengi ni wanaume kuwa na ‘michepuko’ mingi jambo linalofanya wapoteze nguvu nyingi huko na kurudi nyumbani wakiwa wamechoka.


Shakinyau aliyasema hayo jana jijini Mwanza katika semina kwa waandishi wa habari na Jukwaa la Tanzania la Mawasiliano ya Afya kwa watu wazima linalolenga kuleta mabadiliko chanya ya tabia kwa jamii.

Alisema wanaume wengi wamekuwa wakilalamikia wake zao kujifungua watoto wengi wa kike kuliko wa kiume, wakati wao ndio wanasababisha hali hiyo kutokea.

“Ni kweli watoto wa kike katika ndoa wanazaliwa wengi kuliko wa kiume, hata takwimu zilizopo zinaonyesha hivyo hivyo, sasa kwa maelezo ya awali nasema wanapaswa kutulia kwenye ndoa zao.

“Ukiwa na michepuko huwezi kupata mtoto wa kiume ndani ya ndoa maana utarudi nyumbani ukiwa na uchovu wakati nguvu kubwa umeiacha nje ya ndoa na ndio unapata mtoto jinsia ya kike.

“Pili wanapaswa kutambua unapokuwa na uchovu kisha ukafanya tendo lile, mbegu za kike zinakuwa na mbio kuliko za kiume, hivyo nawashauri wanaume waende vituoni ili wapate elimu na watajua lini na wakati gani wa kupata mtoto wa kiume.

“Pia tambueni kuwa mimba nyingi zinazotoka ni za watoto wa kiume, ujauzito wa mtoto wa kiume hauna uvumilivu pale mimba inapopata misukosuko,” alisema Shakinyau.



ENDELEA KUSOMA HABARI HII <<HAPA>>
Na Benjamini Masese - Mtanzania Mwanza

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527