DALADALA ZAGOMA MBEYA


 Madereva wa daladala wa jijini Mbeya leo Jumatatu Machi 18, 2019 wamegoma kutoa huduma ya usafiri kwa shinikizo la kutaka Bajaji zisipite barabara kuu.

Mwandishi wa habari hizi amefika kituo cha Uyole na Makasin na kushuhudia umati wa watu waliokwama kutokana na kukosekana usafiri huo.

Hata hivyo, usafiri ambao unatumika kwa sasa ni bodaboda, gari ndogo za kubeba mizigo maarufu ‘kirikuu’, bajaji pamoja na Noah.

Kutokana na mgomo huo Jeshi la polisi kikosi cha usalama barabarani limefika kwenye vituo kutoa msaada kwa wanafunzi kwa kusimamisha mabasi yanayotoka Kyela na Iringa ili kuwasafirisha wanafunzi kwa gharama ya Sh200.

Kwa mujibu wa Issa Kinyunyu dereva wa daladala za Nsalaga/ Stend kuu amesema wataendelea na huduma ya usafirishaji baada ya kukaa kikao na Mkuu wa Mkoa katika viwanja vya Ruanda Nzovwe.

Na Ipyana Samson - Mwananchi

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527