MHUBIRI SHOGA KUAPISHWA RASMI KUWA KASISI WA KANISA LA ANGLIKANA


Wafuasi wengi wa dini za kikristo katika bara la Afrika wamezidi kushikilia msimamo mkali wa kuwataka wahubiri na mapadri/kuhani kuzingatia maadili na mafunzo ya biblia ndipo waweze kuwaelekeza kondoo wao kwa njia inayofaa.

 Kinyume na matarajio yao, kuna dhana kuwa wengi wa wahubiri hawa wameasi njia hiyo na kuchagua ma maadili watakayofuata na kuacha yale wanahisi hayawafai katika maisha yao ya kila siku. 

Mchungaji Jide Macaulay kutoka nchini Uingereza, ambaye amejianika waziwazi kama shoga, amewatangazia wafuasi wake wa mtandao wa Instagram kuwa, hivi karibuni ataapishwa rasmi kama kuhani/Kasisi kwenye ujumbe aliounakili katika ukurasa wake.
 Mhubiri huyo mwenye asili ya Nigeria, alifichua kuwa sherehe hiyo itafanyika katika kanisa la Uingereza mwezi wa Juni, 30 2019, huku hata akiwaalika wafuasi wake kuhudhuria hafla hiyo.

 "Nina furaha kuu kuwajuza ujumbe huu, nitaapishwa kama padri wa Church of England mnamo Juni,30 2019," Jide alisema. 

Ujumbe huo ulizua mgawanyiko kati ya wafuasi wake, baadhi yao wakigutushwa huku wengine wakimtaja kama mchungaji mnafiki. 

Ujumbe wa Mchungaji huyoMchungaji Jide

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post