MBOWE AONGOZA KIKAO CHA VIONGOZI WA VYAMA 10 VYA UPINZANI TANZANIA


Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe jana March 27, 2019  ameongoza kikao cha viongozi wa vyama 10 vya upinzani nchini na wanasiasa waandamizi.


Kikao hicho kilifanyika saa chache baada ya polisi kuzuia mkutano wa ACT uliokuwa ufanyike ukumbi wa PR Temeke kwa kile kilichoelezwa kuwa wamepata taarifa kuwa kuna wanachama wa CUF ambao walitaka kufanya vurugu.


Mmoja wa watu walioudhuria kikao hicho alidokeza kuwa kilijadili juu ya vyama hivyo kushirikiana katika nyanja mbalimbali.

“Kikao kilijadili mambo mengi ya kushirikiana, tumejadili suala la Sheria mpya ya Vyama vya Siasa, Uchaguzi wa Serikali za Mitaa ambao utafanyika mwaka huu na tisho la kufutwa kwa ACT,” kilidokeza chanzo hicho.

Kilisema ushirikiano huo utaenda mbali zaidi kadiri muda utakavyoenda, yote ikiwa ni kusimamia misingi ya demokrasia.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527