FAMILIA YA LOWASSA NAYO YAREJEA CCM...FREDY LOWASSA AZUNGUMZA

Mamia ya wakazi wa Arusha wamekusanyika uwanja mdogo wa Arusha kumsubiri Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa ambaye amerejea Chama cha Mapinduzi (CCM).

Lowassa aliyetimkia Chadema akitokea CCM ambako alipitishwa kugombea urais katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2015, Mei mosi, 2019 alitangaza kurudi CCM na leo Jumamosi Mei 9, 2019 anarejea nyumbani kwake, Monduli mkoani Arusha.

Watu hao wakiwepo familia ya Lowassa, wakiongozwa na mtoto wake, Fred Lowassa wamesema wamerejea nyumbani CCM na Lowassa.

Fred ambaye naye alijiunga na Chadema baada ya baba yake kutimkia Chadema Julai 28, 2015, amesema familia yote ya Lowassa imerejea nyumbani CCM.

"Kama alivyosema mzee amerudi nyumbani na sisi kama familia tumerudi kumuunga mkono" amesema Fred leo Jumamosi Machi 9, 2019 jijini Arusha.

Amesema anajisikia vizuri kurudi nyumbani kuendelea kushirikiana na rafiki zake ambao aliwaacha CCM na ambao bado wapo Chadema.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post