Picha : WAFANYAKAZI WA DAWASA WASHIRIKI MAADHIMISHO YA SIKU YA WANAWAKE DUNIANI


Wanawake ambao ni Wafanyakazi wa Mamlaka ya MajiSafi na MajiTaka Dar es Salaam (DAWASA) leo wameungana na akinamama wa jijini Dar es Salaam kuadhimisha siku ya wanawake duniani iliyofanyika katika ukumbi wa Mlimani City. Wafanyakazi hao waliingia na bango lenye ujumbe wa kumshukuru rais Dkt John Pombe Magufuli kwa kuweza kumtua mama ndoo kichwani huku wakiwa wamebeba ndoo ya maji ikiwa ni ishara.


Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Paul Makonda akitoa hotuba yake katika maadhimisho ya siku ya wanawake Duniani iliyofanyika katika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam ambapo katika ujumbe wake aliishukuru Mamlaka ya MajiSafi na MajiTaka kwa kuweza kufika asilimia 60 ya utoaji wa huduma ya maji kwa wakazi wa Dar es Salaam na Pwani. 

Pia katika salamu zake Mhe Makonda amewataka akinamama wote kuacha kuwa mstari wa nyuma katika kufanyakazi bali wajitokeze katika kupigania haki zao kwa usawa bila kujali jinsia yao. Picha zote na Cathbert Kajuna - Kajunason/MMG.

Wafanyakazi wa DAWASA wakifuatilia hotuba ya mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam ambaye alikuwa ni mgeni rasmi katika maadhimisho hayo.
Wafanyakazi wa DAWASA wakifuatilia hotuba.
Akinamama wa jiji la Dar es Salaam walifurika katika ukumbi wa Mlimani City kuhudhuria katika maadhimisho ya siku ya wanawake duniani.
Mwimbaji Stara Thomas akitoa burudani
Akinamama kutoka nchini Kenya ambao waliungana na wenzao katika maadhimisho ya siku ya mwanamke duniani.
Msanii Mrisho Mpoto akitoa ujumbe kwa akinamama wakati wa maadhimisho ya siku ya wanawake duniani.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post