WABUNGE WA CHADEMA WAPATA DHAMANA

Wabunge wa Chadema, Suzan Kiwanga (Mlimba), Peter Lijualikali wa Kilombero na wenzao saba wamepata dhamana baada ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Morogoro kutupilia mbali maombi ya upande wa mashtaka ya kupinga dhamana yao.

Wabunge hao pamoja na wenzao, wamepata dhamana baada ya kusota rumande kwa takriban wiki mbili tangu walipofikishwa mahakamani hapo.

Wabunge hao na wenzao wapewa dhamana baada ya hakimu mkazi mfawidhi wa mahakama hiyo Elizabert Nyembele, anayesikiliza kesi hiyo kupitia hoja za upande wa mashtaka za kupinga dhamana na zile za upande wa utetezi zilizoeleza upungufu ya maombi hayo.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post