BASI LILILOBEBA WANAFUNZI LAGONGA TRENI TANGA,MMOJA AFARIKI,MAJERUHI 30 | MALUNDE 1 BLOG

Saturday, March 16, 2019

BASI LILILOBEBA WANAFUNZI LAGONGA TRENI TANGA,MMOJA AFARIKI,MAJERUHI 30

  Malunde       Saturday, March 16, 2019

 Mtu mmoja amefariki papo hapo na wengine 30 kujeruhiwa baada ya basi aina ya Coaster lililokuwa limewabeba wanafunzi kugonga treni katika njia panda ya mtaa wa Dolphine jijini Tanga.

Basi hilo lililokuwa limebeba wanafunzi wachezaji pamoja na washangiliaji zaidi ya 30 liliweza kuburuzwa umbali wa mita 50 kutoka eneo ilipotokea ajali.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Tanga, Edward Bukombe akizungumzia ajali hiyo iliyotokea leo Ijumaa Machi 15, 2019 amemtaja aliyefariki katika ajali hiyo kuwa ni kondakta wa basi hilo ambaye jina lake halijatambulika mara moja.

Majeruhi waliofikishwa hospitali ya Mkoa wa Tanga ya Bombo ni wanafunzi 30 ambapo 19 kati yao hali zao si nzuri na madaktari wanaendelea na kuwapa matibabu.

Na Burhani Yakub, Mwananchi 
Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post