MTANZANIA AELEZA ALIVYONUSURIKA KUFA KWENYE AJALI YA NDEGE ILIYOUA ABIRIA WOTE LEOBaada ya taarifa za ndege aina ya Boeing 737 ya Shirika la Ndege la Ethiopia ambayo ilikuwa na watu 157, kuanguka muda mfupi baada ya kupaa, na watu wote waliopo kwenye ndege hiyo kupoteza maisha, raia mmoja wa Tanzania ameeleza namna alivyopishana na ajali hiyo.

Kufuatia taarifa hiyo, Mtanzania, Antu Mandoza ambaye pia ni mjasiriamali wa urembo na tasnia ya habari, ameeleza namna alivyonusurika katika ajali hiyo iliyotokea asubuhi ya leo.


Katika ukurasa wake wa Twitter amesema kuwa alinusurika kukata tiketi katika ndege hiyo kabla ya kubadili safari ya Addis Ababa na baada ya kushuka ndipo alipokutana na taarifa hizo mbaya huku akipokea ujumbe mwingi na simu kutoka kwa ndugu, jamaa na marafiki waliotaka kujua hali yake.

Kupitia ukurasa wake wa Twitter ameandika ujumbe unaosomeka: 

"I almost took the Ethiopian plane that crashed today I changed the route to Addis, I’m just landing and seeing the news and so many calls from the few people who knew I’m traveling with Ethiopia worried . God is good . Ningekua marehemu saivi. Mungu mkubwa".


I almost took the Ethiopian plane that crashed today I changed the route to Addis, I’m just landing and seeing the news and so many calls from the few people who knew I’m traveling with Ethiopia worried . God is good . Ningekua marehemu saivi🤭. Mungu mkubwa.

118 people are talking about this
Habari zilizothibitishwa na Shirika la ndege la Ethiopia zinasema kwamba ndege hiyo ilikuwa ikitoka Ethiopia kwenda Nairobi, na ilipata hitilafu angani na kupelekea kuanguka kwake.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post