UWANJA WA TAIFA KUFUNGWA


Uwanja wa taifa
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe amesema uwanja mkuu wa taifa utafungwa kwa muda ili kupisha maandalizi ya fainali za michuano ya AFCON kwa vijana chini ya miaka 17.

Akiongea leo Februari 14,2019 kwenye mkutano na wanahabari uliofanyika makao makuu ya shirikisho la soka nchini (TFF), Mwakyembe amesema ili eneo la kuchezea na miundombinu mingine ya uwanja huo iwe kwenye ubora ni lazima ipunguziwe majukumu.

''Tutaufunga uwanja wetu wa taifa kwa muda wa mwezi mmoja kabla ya mashindano kuanza ili kuweka sawa ubora wa miundombinu yake kwaajili ya michuano hiyo mikubwa Afrika'', amesema.

Michuano hiyo inaanza 14–28 April 2019 hivyo uwanja wa taifa utafungwa kuanzia Machi 14.

Kwasasa uwanja huo unatumika kwa mechi za ligi kuu soka Tanzania bara zinazohusisha vilabu vya Yanga, Simba pamoja na Azam FC inapocheza na timu hizo. Pia Simba inautumia katika michuano ya klabu bingwa Afrika.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527