WAZIRI MKUU AMUONYA MKUU WA WILAYA NA MKURUGENZI KWA USHIRIKINA BIHARAMULO


Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amemtaka mkuu wa Wilaya ya Biharamulo mkoani Kagera Sada Malunde na mkurugenzi wa halmashauri hiyo, Wende Ng’ahara wamalize tofauti zao na wasipojirekebisha atamshauri Rais John Magufuli kufanya uamuzi mwingine dhidi yao.



Amesema kutokuelewana kwa viongozi hao ambao wakati mwingine wanatuhumiana kufanyiana vitendo vya kishirikina kumesababisha kuzorota kwa shughuli za maendeleo katika Wilaya hiyo.

Waziri Mkuu ametoa kauli hiyo leo Jumatano Februari 20, 2019 wakati akihutubia wananchi kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika uwanja wa mpira wa shule ya msingi Nyakanazi kijiji cha Nyakanazi, Biharamulo mkoani Kagera.

Amesema viongozi hao kutoelewana ni mfano mbaya kwa watumishi walio chini yao, kuwataka kujirekebisha mara moja kwa kuwa wameaminiwa na Serikali kuliongoza eneo hilo na si kuwachanganya wananchi.

“Mliletwa hapa kuiwakilisha Serikali na kusimamia maendeleo ya wananchi nyie mnagombana.”

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527