DC MBONEKO ATEMBELEA KITUO CHA AFYA TINDE...ATAKA DIRISHA LA WAZEE NA CHF

Mkuu wa wilaya ya Shinyanga, Jasinta Mboneko ametembelea kituo cha Afya Tinde kilichopo katika halmashauri ya wilaya ya Shinyanga ili kujionea hali halisi ya utoaji huduma kwenye kituo hicho.

Akizungumza wakati wa ziara hiyo leo Februari 21,2019,Mkuu huyo wa wilaya amesema serikali inaendelea kuboresha huduma za afya kwa wananchi na kusisitiza kuwa hakuna upungufu wa dawa.

Mboneko ameagiza watumishi wa afya katika kituo hicho kutenga eneo/dirisha kwa ajili ya Wazee na Mfuko wa Afya ya Jamii (CHF) baada ya kubaini kuwa bado kuna mapungufu hayo kwenye kituo hicho.

Pia amewataka watoa huduma kuepuka kutoa lugha mbaya kwa wagonjwa badala yake wawapatie huduma kama inavyotakiwa. 
Kushoto ni Afisa Mtendaji kata ya Tinde, Claudia Kimaro akimwongoza Mkuu wa wilaya ya Shinyanga, Jasinta Mboneko (katikati) kutembelea kituo cha afya Tinde.Wa tatu kutoka kulia ni Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Shinyanga, Azza Hilal Hamad.Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga, Jasinta Mboneko (katikati) akiwa katika eneo Huduma za tiba na Matunzo (CTC) kwenye kituo cha Afya Tinde. Kulia ni Kaimu Mganga Mfawidhi wa kituo hicho Mbabasi Jacenti akielezea kuhusu huduma zinazotolewa CTC.  
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga, Jasinta Mboneko akiingia katika chumba cha maabara.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga, Jasinta Mboneko akiwa katika chumba cha maabara.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga, Jasinta Mboneko akiwa katika wodi ya wanaume.
Kaimu Mganga Mfawidhi wa kituo cha afya Tinde ,Mbabasi Jacenti akimweleza jambo Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Shinyanga, Azza Hilal Hamad.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga, Jasinta Mboneko akiwa chumba cha wahudumu kwenye wodi ya akina mama.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga, Jasinta Mboneko akiwa kwenye wodi ya akina mama
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga, Jasinta Mboneko akizungumza baada ya kutembelea kituo cha afya Tinde.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527