SIMBA YAIADHIBU YANGA


Meddie Kagere akijaribu kumiliki mpira mbele ya Vicent Andrew

Mabingwa watetezi wa Ligi kuu soka Tanzania Bara klabu ya soka ya Simba imeibuka na ushindi wa bao 1-0, dhidi ya Yanga kwenye mchezo wa watani wa jadi uliopigwa leo Februari 16 kwenye dimba la taifa Dar es salaam.

Simba imebeba pointi zote tatu kupitia bao la Meddie Kagere ambaye alifunga dakika ya 72 akipokea pasi safi kutoka kwa nahodha John Bocco na kumalizia kwa kichwa.

Baada ya ushindi wa leo Yanga imeendelea kubaki kileleni mwa msimamo wa ligi, ikiwa na pointi 58 wakati Simba wanajivuta kutoka nafasi ya 5 hadi ya 3 wakiwa na pointi 39.

Tayari Yanga imeshacheza mechi 24 huku Simba wakicheza mchezo wao wa 16 msimu huu katika ligi ambayo ipo kwenye mzunguko wa 27 kwaa baadhi ya timu.

Kwa upande mwingine klabu ya Yanga ambayo imetoka kuadhibiwa na TFF kwa kuingia uwanjani kwa kutumia mlango usio rasmi kwenye mchezo dhidi ya Coastal Union, itakuwa inasubiri adhabu hiyo tena baada ya leo kuingia tena uwanja wa taifa kwa kutumia mlango usio rasmi.

Katika faini iliyopita Yanga ilitozwa kiasi cha shilingi laki mbili (200,000/=).

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527