Wednesday, February 27, 2019

SHIRECU YAPUNGUZA WATUMISHI NA KUWALIPA STAHIKI ZAO

  Malunde       Wednesday, February 27, 2019

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI 

Katika kipindi cha miezi kumi iliyopita tangu kuchaguliwa kwa bodi mpya ya chama kikuu cha ushirika mkoa wa Shinyanga chini ya Mwenyekiti LUHENDE RICHARD LUHENDE,kimefanikiwa kupunguza wafanyakazi takribani 12 na kulipwa stahiki zao.
Aidha kiasi cha Tshs 95,155,118.00 kimeweza kutumika kuwalipa watumishi hao.


Watumishi hao wamepunguzwa kama jitihada za chama kikuu cha ushirika mkoa wa Shinyanga  katika kujiimarisha kiutendaji na ni mkakakti endelevu wa Kupunguza na kuwalipa stahiki zao watumishi ambao wamehudumu kwa muda mrefu katika chama hicho.

Sambamba na hilo Bodi ya SHIRECU (1984) ltd imeajiri menejimenti mpya ya wakuu wa idara za Uhasibu,Utumishi,Tehama na Ukaguzi wa ndani ili kuleta mabadiliko  ya kiutendaji katika union.

Imetolewa na: 

Idara ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano 
Shinyanga Regional Cooperative Union (SHIRECU(1984)LTD). 
26.02.2019.

Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post