PAPA FRANCIS KUANZA ZIARA RASMI FALME ZA KIARABU

Ziara hiyo ya kiongozi wa kanisa Katoliki duniani ni ya kwanza kuwahi kufanywa na kiongozi wa kanisa hilo kwenye rasi ya Uarabuni.

 Lengo ni kufungua ukurasa mpya katika uhusiano baina ya wakristo na Waislamu.

Mrithi wa mfalme wa Abu Dhabi Sheikh Mohammed bin Zayed Al Nahyan alimpokea Papa Francis kwenye uwanja wa ndege akiwa na tabasamu huku akiongozana na mawaziri wake. 

Imam mkuu wa msikiti maarufu wa Al-Azhar wa nchini Misri, Ahmed el Tayeba pia alikuwapo uwanja wa ndege kumlaki Baba Mtakatifu.

 Leo hii Papa Francis na imam el Tayeb watahutubia kwenye mkutano utakaohudhuriwa na wawakilishi wa dini zote. 

Hapo kesho Papa Francis ataongoza misa itakayokuwa ya kwanza kuongozwa na baba mtakatifu kwenye rasi ya Uarabuni. Waumini wapatao 135,000 wanatarajiwa kuhudhuria misa hiyo ya hadharani.

Chanzo:Dw

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post