BENKI YA NMB YAMWAGA MISAADA KUSAIDIA SHULE MKOANI KATAVI


Benki ya NMB imekabidhi msaada wa vifaa kwa ajiri ya shule za Sekondari na msingi vyenye thamani ya shilingi milioni 40 kwa shule za Sekondari tano na tatu za msingi mkoani Katavi.

Hafla za makabidhiano hayo zilifanyika jana katika viwanja vya shule ya Sekondari ya Rungwa katika Manispaa ya Mpanda na kuhudhuriwa na mwakilishi wa Mkuu wa Mkoa wa Mkoa wa Katavi ambae ni Mkuu wa Wilaya ya Mpanda Lilian Matinga na wakuu wa Wilaya za Tanganyika , Mlele, Meya wa Manispaa ya Mpanda , Wenyeviti wa Halmashauri na wakurungezi wa Halmashauri hizo.

Vifaa hivyo vilivyokabidhiwa ni pamoja na mabati 1,248 ambayo yatatumiwa kwa ajiri ya ujenzi wa vyumba vya madarasa katika sekondari za Mizengo Pinda katika Wilaya ya Mlele , Simbesa sekondari , Bulamata Sekondari zilizopo katika Wilaya ya Tanganyika na Sekondari ya Kakese katika Manispaa ya Mpanda .

Shule za Msingi zilizonufaika na msaada huo ni Katavi katika Manispaa ya Mpanda , Luchima na Ikulwe katika Halmashauri ya Mpimbwe .

Pia Benki ya NMB imetoa msaada wa wa viti na meza za kusomea 62 kwa ajiri ya Sekondari ya Rungwa ambayo ilikuwa inakabiliwa na tatizo kubwa la upungufu viti na meza za kusomea 402 hali ambayo ilikuwa ikiwafanya wanafunzi washindwe kusoma kwa raha.

Akizungumza wakati akikabidhi msaada huo,   Meneja wa NMB Kanda ya Nyanda za Juu Straton Chilongola alisema kuwa msaada huo wameutowa ni katika kuunga mkono juhudi za Serikari kwa jamii ya Kitanzania ,na kwa kuwa Benki ya NMB imeguswa na uhitaji wa shule hizo wamejisikia faraja kuzisaidia .

Chilongola alisema kwa mwaka 2018 NMB imetenga zaidi ya shilingi bilioni 1 kwa ajiri ya kuchangia maendeleo ya jamii ikiwemo kusidia sekta ya afya na elimu ,Kiasi hiki kinaifanya kuwa benki ya kwanza katika kuchangia maendeleo kuliko benki yoyote hapa nchini.

"Kiasi hiki kinaweza kuonekana si kikubwa sana lakini kimekuwa msaada mkubwa kwa jamii hasa katika sekta ya afya na elimu kwani vifaa vya Afya na Elimu vimekuwa ni changamoto kubwa katika katika Hospitali na vituo vya afya vingi na shule zetu hapa nchini", alisema Meneja huyo wa Kanda.

Alieleza kuwa NMB imezifikia Wilaya zote nchini kwa asilimia 100 na wanaendelea kuboresha huduma za kibenki kwa njia ya mitandao ili kuwafikishia huduma za kibenki wananchi wengi zaidi.

Benki hiyo itaendelea kuunga mkono juhudi za Serikali na wadau wake wakubwa katika kuhakikisha kuwa changamoto za jamii zinapatiwa ufumbuzi katika kujenga elimu bora kwa jamii ya Kitanzania.

Mwakilishi wa Mkuu wa Mkoa, Mkuu wa Wilaya ya Mpanda Lilian Matinga alisema Benki ya NMB imekuwa karibu sana na Serikali katika kusaidia maendeleo hapa nchini .

Alisema msaada huo waliotoa kwa shule hizo katika Mkoa wa Katavi utasaidia katika kusukuma maendeleo ya elimu hivyo aliomba wadau mbalimbali waweze kusaidia kwenye elimu kama ambavyo walivyofanya benki hiyo kwani changamoto ya elimu na afya bado ni kubwa .

Mkuu wa Wilaya ya Mlele,  Rachael Kasanda aliipongeza benki ya NMB kwa kutoa msaada huo na kubainisha kuwa wameonyesha jinsi wanavyoijali jamii ya Wanzania kwani fedha hizo walizotumia shilingi milioni 40 wangeweza kuziingiza kwenye biashara yao.

Afisa Elimu Taaluma wa Manispaa ya Mpanda Raphael Mkupi alisema msaada wa viti na meza uliotowa na NMB kwa shule ya Sekondari ya Rungwa utasaidia sana kupunguza tatizo la upungufu wa viti na meza kwa wanafunzi hapo shuleni yenye kuanzia kidato cha kwanza hadi cha sita ambapo wanafunzi 62 kati ya 402 ambao walikuwa hawapati huduma ya viti na meza sasa watapata huduma ya samani nzuri kutoka Benki ya NMB.

Na Walter Mguluchuma - Katavi.
Meneja wa benki ya NMB Kanda ya Nyanda za Juu Straton Chilongola (wa nne kutoka kushoto pichani) akimkabidhi bando za bati katika shule ya sekondari Rungwa Manispaa ya Mpanda mkoani Katavi Mkuu wa wilaya ya Mpanda Lilian Charles Matinga  (wa tatu kutoka kushoto pichani) msaada huo ni mwendeleza wa NMB kuchangia katika sekta ya elimu na afya -Picha na Walter Mguluchuma.

Mkuu wa Wilaya ya Mpanda Lilian Charles Matinga (katikati) akikata utepe wakati akipokea madawati 62 kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Katavi Amos Makalla.

Mkuu wa Wilaya ya Mpanda Lilian Charles Matinga (katikati) akipokea madawati 62 kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Katavi Amos Makalla.

Meneja wa benki ya NMB Kanda ya Nyanda za Juu Straton Chilongola akielezea kuhusu madawati waliyokabid
hi.
Picha na Walter Mguluchuma.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post