NAPE NNAUYE AJIUZULU UENYEKITI KAMATI YA BUNGE



Nape Nnauye
Katibu wa Bunge, Ndugu Stephen Kagaigai amethibitisha kupokea barua ya mbunge wa Mtama Mh. Nape Nnauye kujiuzulu nafasi ya Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii.

Kagaigai amesema leo Jumatatu Februari 04, 2019 Nape ameandika barua kwenda kwa Spika wa Bunge la Tanzania, Job Ndugai ya kujiuzulu nafasi hiyo na tayari spika amempatia nakala ya barua hiyo.

''Ni kweli nimeiona barua aliyomwamndikia Spika na mimi nimepata nakala yangu kwahiyo ni kweli amejiuzulu labda awe na mawazo mengine'', amesema.

Hata hivyo www.eatv.tv imemtafuta Nape Nnauye ambaye alipokea simu yake kisha kusema yupo kwenye kikao hawezi kuendelea na maongezi. ''Nipo kwenye mkutano siwezi kuongea'', alisema.

Machi mwaka 2017, Nape aling’olewa kwenye nafasi ya Uwaziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo ambayo sasa ipo chini ya Waziri Harrison Mwakyembe.
Chanzo-EATV

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527