WAZIRI AZINDUA SHINDANO LA WANAWAKE WENYE MAKALIO MAKUBWA 'MAWOWO' KUVUTIA WATALII


Wanawake wenye makalio makubwa (picha kutoka mtandaoni)
Waziri waziri wa Utalii Godfrey Kiwanda akizindua shindano la kusaka mwanamke mwenye makalio makubwa
Waziri wa Utalii Godfrey Kiwanda akiwa na warembo wa Uganda

Wizara ya Utalii nchini Uganda imewaainisha wanawake wenye umbile namba 8, makalio makubwa na miguu minene kuwa kivutio cha utalii nchini humo.

Akizindua shindano la "Miss Curvy" ambalo litaonyesha shepu halisi ya wanawake wa Kiafrika ambalo litawawezesha wanaweke kuonyesha makalio yao makubwa, Februari 5,2019, Waziri wa Utalii Godfrey Kiwanda alisema Uganda ina wanawake warembo wenye shepu za kuvutia na hivyo serikali itawatumikia wanawake hao kukuza sekta ya utalii.

 Gazeti la Daily Monitor, lilisema kuwa wanawake wote wenye figa nzuri watashiriki katika shindano la kubaini nani ndiye aliye na umbile bora zaidi na atachaguliwa kuwakilisha nchi hiyo. 

"Tuko na wanawake warembo sana humu nchini, wenye shepu ya kudondosha mate kwa kila mwanaume, mbona tusiwatumie hawa watu kukuza sekta ya utalii humu nchini?" Waziri Kiwanda alisema.

Ann Mungoma ambaye ni mwandalinzi wa shindano hilo alisema, sekta ya utalii itaboreshwa punde tu mwanamke mwenye figa na makalio ya kuvutia atakapochaguliwa.

 Mungoma alisema Waafrika wanapaswa kuelewa kuwa watu wanene pia wanaweza kuwa warembo wala sio wembamba pekee. 

 "Miss Curvy in tamasha ambalo litaonyesha shepu halisi ya wanawake wa Kiafrika, tamasha hilo ni la kipekee ambalo litawawezesha wanaweke kuonyesha makalio yao makubwa, umbile namba 8 na kila kitu walichojaliwa nacho mwilini mwao," Mungoma alisema. 

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527