MWANAMKE AMUUA KWA PANGA MTOTO WA MAMA ALIYEDAI KAZAA NA MMEWE

Mwanamke aliyejulikana kwa jina la Paskazia Andrew Sindano (17) anashikiliwa na jeshi la polisi mkoa wa Shinyanga kwa tuhuma za kumuua kwa kumkata panga kichwani mtoto Kashindye Mgemagiko (03) anayedaiwa kuzaliwa na mama mwingine mwenye mahusiano ya kimapenzi na mmewe. 

Kwa Mujibu wa taarifa kwa vyombo vya habari kutoka kwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP Simon Haule,tukio hilo limetokea Februari 15,2019 majira ya saa 12 jioni katika kitongoji cha Emalaupena,kijiji cha Misayu kata ya Ubagwe halmashauri ya wilaya ya Ushetu. 

“Chanzo cha tukio hili ni wivu wa kimapenzi kwa kuwa mama wa mtoto aliyeuawa inasemekana alikuwa na mahusiano ya kimapenzi na mume wa Paskazia na kupelekea kuzaliwa mtoto huyo”,ameeleza Kamanda Haule. 

“Mbinu iliyotumika ni kumkata panga kichwani nje ya nyumba yake,tumemkamata na tutamfikisha mahakamani mara moja”,ameongeza. 

Aidha Kamanda Haule amewataka wananchi kuacha kujichukulia sheria mkononi na badala yake wapeleke malalamiko,kero na migogoro yao hususani ya kimapenzi katika ofisi ya serikali ya kijiji na mabaraza ya wazee ili kuepuka vitendo vya kinyama. 

Na Kadama Malunde – Malunde1 blog

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post