JAMAA AJIUA KWA KUJIRUSHA KWENYE GARI KISA MCHUMBA WAKE KACHEPUKA NA RAFIKI YAKE | MALUNDE 1 BLOG

Saturday, February 23, 2019

JAMAA AJIUA KWA KUJIRUSHA KWENYE GARI KISA MCHUMBA WAKE KACHEPUKA NA RAFIKI YAKE

  Malunde       Saturday, February 23, 2019
Jamaa mmoja mjini Naivasha nchini Kenya amejitoa uhai baada ya kugundua kuwa mpenzi wake alikuwa na uhusiano wa kimapenzi na rafiki yake wa karibu. 

 Kwa mujibu wa  shuhuda wa tukio hilo, Samuel Kimani, jamaa huyo aliruka mbele ya lori lililokuwa likiendeshwa kwa mwendo wa kasi katika barabara kuu ya Nakuru kuelekea Nairobi siku ya Ijumaa.

Taarifa za The Standard Ijumaa Februari 22,2019 zinaeleza kuwa jamaa huyo aliacha kijikaratasi kwenye mfuko wake ambapo alikuwa ameelezea sababu yake kujitoa uhai ambapo alimlaumu mpenzi wake kwa kutokuwa mwaminifu katika uhusiano wao wa kimapenzi.

Alidai kuwa aliamua kuchukua hatua hiyo baada ya mpenzi wake waliopanga kufunga ndoa kwa pamoja kumsaliti kwa kushiriki mapenzi na rafiki wake wa karibu.

 "Alielezea kwenye kijikaratasi hicho jinsi alivyokutana na mpenzi wake na wawili hao walikuwa wanapanga kufunga pingu za maisha hivi karibu ila alimpata mpenziwe akishiriki mapenzi na rafiki wake wa karibu," Kimani alisema.

 " Marehemu aliwaonya wawili hao dhidi ya kuhudhuria mazishi yake kwani ni wao walimpelekea yeye kujitoa uhai," Kimani aliongezea.

 Afisa mkuu wa Naivasha Samuel Waweru alithibitisha kisa hicho na kusema mwili wa mwendazake ulipelekwa katika chumba cha kihifadhi wafu cha hospitali ya kata ndogo ya Naivasha. 

Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post