HUYU NDIYO JAMAA ANAYEOA MAPACHA WAWILI WANAOFANANA...HULALA NAO KITANDA KIMOJA

Mapacha Anna na Lucy na mchumba wao Ben Bryne


Mapacha Anna na Lucy
Mapacha wanaofahamika kufanana ulimwenguni mzima wamefichua kwamba wanapanga kuolewa kwa mpenzi mmoja aitwaye Ben Bryne  hivi karibuni.

Mapacha hao huwa wanakula pamoja,kuoga pamoja na wana mpenzi mmoja.

Anna na Lucy DeCinque wenye umri wa mia 33 kutoka Perth nchini Australia walisema wao hulala kwenye kitanda kimoja na mpenzi wao na hata hushiriki tendo la ndoa kwa pamoja ambapo kila mmoja huwa anakuwepo wakati mwenzake akishiriki tendo la ndoa na Ben.

Wakizungumza kwenye mahojiano na runinga moja nchini Australia, mapacha hao walisema hawana wivu kati yao na wao kuonyeshwa mapenzi ya dhati na mpenzi wao. 

Kulingana na mapacha hao ambao wanaishi pamoja na mama yao, walisema wanapanga harusi hivi karibuni licha ya serikali ya Australia kutokubali ndoa za mitala.

 "Hakuna wivu kati yetu, mpenzi wetu akimbusu mmoja wetu, atambusu tena mwingine, mpenzi wetu Ben Bryne
 hufurahia mtindo wetu wa kimavazi na hutusifia kila mara, tunampenda sana sisi wote," Mapacha hao walisema. 

Mapacha hao pia walisema wanapanga kupata mimba pamoja na kuzaa watoto wao wakati mmoja. 

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post