MANARA AWAPA DONGO WANA YANGA "NITAACHA KAZI SIMBA JANUARI 2021 TENA KWA HIARI"


Haji Manara
Baada ya kusambaa kwa tetesi nyingi kuwa Afisa Habari wa Simba, Haji Manara yuko mbioni kutemwa katika nafasi yake, mwenyewe ameibuka na kueleza kinagaubaga kuhusiana na taarifa hizo.

Tetesi hizo zilisambaa mara baada ya Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Kampuni ya Simba Sports Club, Mohamed Dewji 'Mo' kuitisha mkutano na wanahabari, Ijumaa Februari 8 kuhusiana na masuala mbalimbali ya klabu hiyo pamoja na maandalizi ya mchezo wa Klabu Bingwa Afrika dhidi ya Al Ahly.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Manara amesema kuwa anafahamu kuwa mashabiki wengi hasa wa Yanga wanapenda asiendelee kuwepo Simba na siku wakisikia ameondoka watamfanyia sherehe kutokana na jinsi anavyowatesa.

"Kuna watu wa Yanga hamu yao nife kabisa!!, nawaumiza sana na siku mtakaposikia sipo kikazi Simba, mtafanya sherehe. Ila nikuhakikishie kuwa Mungu akinipa uhai nitaacha kazi Januari 2021 tena kwa hiari", amesema Manara alipokuwa akijibu 'comment' ya moja ya mfuasi wake.

Pia tetesi za Simba kuachana na Manara zimezidi kutiwa chumvi hasa pale Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi alipotangaza ujio wa nafasi za kazi katika idara mbalimbali hivi karibuni, ambapo watu wenye taaluma hizo watatuma maombi.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post