MKUU WA MAJESHI ATINGA NJOMBE SAKATA LA MAUAJI YA WATOTO


Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama, Jenerali Venance Mabeyo, akiwasili Mkoani Njombe.

Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama, Jenerali Venance Mabeyo ametinga mkoani Njombe na kufanya mkutano wa ndani na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Njombe pamoja na vikosi maalumu vilivyopo mkoani humo kwa ajili ya kuchunguza matukio ya mauaji ya watoto.

Akizungumza na waandishi wa habari mkoani Njombe Mabeyo amesema “vyombo vya ulinzi na usalama vinafanya kazi kwa kushirikiana pamoja na jeshi, na mimi ndiye mwenyekiti wa vyombo vyote vya ulinzi hivyo ninaowajibu na si kwamba jeshi limeingia sasa, hapana hatujafikia hatua ya kuingiza jeshi,”

"Wananchi karibu nchi nzima wamesikia kinachoendelea Njombe, wengine yamewatia hofu lakini si Tanzania tu mpaka nje ya mipaka yetu taarifa zimesambaa,” amesema.

“Kwa hiyo pasiwepo na hofu suala hili ni la kitaifa zaidi, linahusu pengine familia moja moja sababu zinajionesha kabisa ni za kifamilia zaidi,” amesema.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Njombe, Renatha Mzinga amesema watuhumiwa 30 wanashikiliwa kutokana na kuhusika kwao na utekaji na mauaji ya watoto hao.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post