VIJANA WAFARIKI WAKIOGELEA KWENYE LAMBO LA KUJENGEA BARABARA SHINYANGA


Picha haihusiani na habari hapa chini


 Vijana wawili waliofahamika kwa majina ya Mateo Dase (22) mkazi wa Kadoto na Jonas  Pigi (27) wote wakazi wa Kadoto wamefariki dunia baada ya kuzama kwenye maji katika lambo la kitongoji cha Kadoto wakiwa wanaogelea kwenye lambo lililotokana na uchimbaji wa kokoto zilizotumika kujengea barabara itokayo Mjini Shinyanga kwenda Bubiki - Kishapu.

Kwa Mujibu wa Kaimu Kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga ACP Richard Abwao tukio hilo limetokea Februari 14,2019 majira ya saa saa tano asubuhi kijiji cha Kadoto, kata ya Mwalukwa, Tarafa ya Nindo, wilaya ya Shinyanga.

 Kamanda Abwao amesema mazingira ya vifo hivyo ni kwamba Jonas Pigi  alikuwa anafanya juhudi za kumuokoa Mateo Dase aliyekuwa ameshazama ndipo wote wawili wakazama. 

"Juhudi za kuopoa miili ya marehemu kutoka kwenye lambo hilo zimefanyika kwa kushirikiana na Jeshi la Zimamoto na Uokoaji na SHUWASA kwa kuyatoa maji kwenye lambo hilo, miili ya marehemu imekabidhiwa kwa ndugu kwa taratibu za mazishi",amesema.

Na Kadama Malunde - Shinyanga

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527