KIKWETE ATOA NENO KIFO CHA RUGE ' TUMEPOTEZA KIJANA MAHIRI'

Rais mstaafu wa Tanzania, Jakaya Kikwete ameeleza maumivu aliyonayo kufuatia kifo cha Mkurugenzi wa Vipindi na Uzalishaji wa Clouds Media Group, Ruge Mutahaba.

Kupitia akaunti yake ya Instagram, Kikwete ameandika ujumbe maneno yafuatayo:

“Nimelemewa! Nakosa maneno ya kuelezea huzuni na majonzi niliyonayo kwa kifo cha Ruge Mutahaba. 

"Taifa limepoteza kijana wake mahiri, mbunifu na mzalendo wa kweli. Nimepoteza rafiki, mshirika mwaminifu na mtu ambaye amenisaidia kwa mengi ktk uongozi wangu na hata baada ya kustaafu.

"Moyo wangu uko pamoja na wazazi wake, ndugu zake na familia yake katika kipindi hiki kigumu. Namuombea kwa Mola ampe Mapumziko Mema Peponi. Ameen. "

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527