HAYA NDIYO MAJEMBE YA SIMBA NA YANGA LEO

Ikiwa yamebaki takribani masaa machache mchezo kati ya Yanga na Simba kupigwa, vikosi vya timu zote mbili tayari vimeshatoka na kuwa wazi moja kwa moja.

Katika kikosi cha Simba kuna mabadiliko kwenye safu ya ulinzi, baada ya kumuanzisha Zana Coulubaly kwenye eneo la beki wa kulia na kumuacha nje Nicholas Gyan ambaye amekuwa akiaminika kwa mashabiki wengi.


Kikosi cha Yanga, Ramadhan Kabwili, Paul Godfrey, Gadiel Michael, Andrew Vicent, Kelvin Yondan, Abdallah Shaibu, Feisal Salum, Papy Tshishimbi, Herieter Makambo, Amis Tambwe na Ibrahim Ajib.

Kwa upande wa Simba kikosi chao, Aish Manula, Zana Coulibaly, Mohammed Hussein, Juuko Murshid, Pascal Wawa, James Kotei, Clatous Chama, Jonas Mkude, John Bocco, Meddie Kagere na Emmanuel Okwi.
Na THOMAS NG’ITU

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post