Picha : DIJITALI KWA MAENDELEO (OXFAM)YAIBUA CHANGAMOTO NYINGI KATIKA JAMII IKIWEMO YA MAJI



Katibu mkuu Wizara ya maji Profesa Kitila Mkumbo akijibu akizungumza na waraghabishi kutoka mikoa mbalimbali katika mkutano wa Digitali kwa maendeleo ulioandaliwa na Shirika la OxfamTanzani na kufanyika Katika ukumbi wa African Dreams Jijini Dodoma

Naibu waziri wa Elimu William Olenasha akizungumza katika mkutano wa Waraghabishi wa Digitali kwa Maendeleo ulioandaliwa na Shirika la OXFAM Tanzani Jijini Dodoma
Naibu Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia na Mbunge wa Ngorongoro William Olenasha akipita taarifa kupitia simu yake ya mkononi katika mkutano wa Digitali kwa Maendeleo ulioandaliwa na Shirika la Oxfam Jijini Dodoma
Sabore Ngarusi Kutoka wilayani Ngorongoro akiuliza swali kwa Katibu Mkuu wizara ya Maji Profesa Kitila Mkumbo kwamba wizara hiyo imejipangaje kuondoa taizo la maji wilayani humo.
Mbunge wa Viti maalum Dodoma Mhe. Fatuma Tawfiq akifuatilia mjadala katika mkutano huo wa Digitali kwa Maendeleo Jijini Dodoma
Mbunge wa Mbogwe mkoa wa Geita Mhe. Maselle akifuatilia mjadala kwa makini
Mbunge wa Mtwara vijijini Mhe. Hawa Ghasia akichangia mjadala katika Mkutano wa Digitali kwa Maendeleo ulioandaliwa na Shirika la Oxfam Nchini Jijini Dodoma
Mbunge wa Viti maalum Dodoma Mhe. Fatuma Tawfiq akichangia mada katika mkutano huo wa Digitali kwa Maendeleo Jijini Dodoma
Katibu mkuu Wizara ya maji Profesa Kitila Mkumbo akifuatilia mjadala Digitali kwa Maendeleo kwa makini Jijini Dodoma
Jimmy Luhende Kutoka Shirika la ADLG. akichangia mada katika mkutano wa waraghabishi wa Digital Kwa maendeleo ulioandaliwa na Shirika la Oxfam Tanzania. 
Naibu Waziri wa Elimu Willium Olenasha akiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi kutoka katika Shirika la Oxfam Tanzania
Naibu waziri wa Elimu Willium Tate Ollenasha akiwa katika picha ya pamoja na viongozi mbalimbali na Waandishi wa habari za mtandaoni Jijini Dodoma katika Mkutano wawaraghabishi Digitali kwa maendeleo

Na Vero Ignatus, Dodoma

Zaidi ya 30% ya miradi ya maji iliyokamilika vijijini haifanyi kazi kwa sababu imekabidhiwa kwa jamii kwani ni tofauti na ile ya mijini ambayo inakabidhiwa kwa Wahandisi au kwa wataalamu wa maji.

Hayo yamesemwa na Katibu mkuu Wizara ya Maji Profesa Kitila Mkumbo alipokuwa katika mkutano wa waraghabishi Digitali kwa maendeleo Jijini Dodoma ulioandaliwa na Shirika la Oxfam Nchini ambapo amesema miradi hiyo inapokabidhiwa kwa wananchi haina uangalizi wa kutosha.

Profesa Mkumbo amesema Kituo kimoja cha maji kinapaswa kuhudumia watu 250 hadi kufikia January 2019 tayari wameshajenga vituo 130,000 vijijini na vinavyofanya kazi,83,000 takribani wananchi 60 mpaka 65 wanapata maji.

Amesema kuwa Madhumuni ya Sheria Mpya ya Rasilimali za Maji Na. 11/2009 ni kuhakikisha kuwa Rasilimali za Maji hapa nchini zinatunzwa, zinatumiwa, zinaendelezwa, zinaboreshwa, zinasimamiwa na kudhibitiwa kwa kuzingatia kanuni.

Amesema kuwa Sheria mpya ya Maji iliyopitishwa inagusia vipengele viwili uanzishwaji wa wakala wa maji vijijini adhabu kwa watu wanaoharibu miundombinu ya maji.

Amezitaja Wilaya ya Ngorongoro iliyopo mkoani Arusha kuwa ni mojawapo yenye changamoto kubwa ya kufikiwa kutokana na Jiografia yake ila hadi sasa (Mb)Mh.William Ollenasha Ameshafanya usanifu vijiji 8 vitanufaika na mradi wa maji.

Akijibu swali lililoulizwa na mmoja wa Waraghabishi kuhusiana na uondoshwaji wa bei za maji Profesa Mkumbo amesema Mchakato wa kupandisha bei ya maji ni shiriki, linaanza na mamlaka ya maji na mara nyingi upandaji wa bei ya maji inategemeana na gharama za uendeshwaji wa mamlaka za maji.

Vilevile ameainisha Takwimu za upatikanaji wa maji kwamba zinazipata kwa aina mbili ambazo ni Miundombinu ya maji ilivyo sambazwa, Kutumia water system kwenye mtandao wa EWURA ambapo Tafiti yake hufanyika kwa kuwapigia wananchi na kuwauliza maswali.

''Kwa mujibu wa Takwimu za mwaka 2017 za NBS zinaonesha 66% ya wananchi wa Tanzania wanapata maji'', alisema Mkumbo.

Kwa upande wake Naibu waziri wa Elimu Sayansi na Yeknolojia na mbunge wa Ngorongoro Willium Olenasha amelishukuru Shirika la Oxfam kwa kutoa mafunzo kwa wananchi namna ya kutumia nyenzo za digitali ili kuleta maendeleo kwa jamii inayowazunguka.

Naibu Waziri wa wa Elimu, Sayansi na Teknolojia William Olenasha amesema kuwa Serikali ipo pamoja na Oxfam pamoja na Waraghabishi katika kuhakikisha kwamba changamoto zinazoibuliwa na wananchi zinatatuliwa na viongozi husika kwa haraka na kwa wakati.

Ameongeza kuwa Nchi nyingi zimesonga mbele kwa kasi kwa sababu ya kutumia teknolojia ya dijitali hivyo Oxfam imekua ikishirikiana na serikali katika shughuli za maendeleo ikiwemo mradi huo wa Dijitali Kwa Maendeleo.

Wakishukuru Shirika la Oxfam kwa mafunzo ya kutumia nyenzo za Digitali kwa maendeleo Lucy Samweli, Diwani viti Maalumu Kata ya Nyasato Geita amesema Kwa kutumia mitandao ya kijamii amepata ushauri kutoka kwa watu mbalimbali wanaosoma anachokituma katika mitandao hiyo na hivyo kuboresha utendaji kazi yake.

Naye Bi Royce Jumanne, Mraghabishi kutoka Kigoma amesema kuwa Kupitia simu zao za mkononi waraghabishi wamefanikiwa kuhamasisha jamii kuchangia madawati ili kuwezesha wanafunzi kusoma katika mazingira mazuri.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527