MKUU WA WILAYA APIGA MARUFUKU VYAKULA KUUZWA CHINI SHINYANGA



Mkuu wa wilaya ya Shinyanga, Jasinta Mboneko amepiga marufuku wafanyabiashara wa vyakula kuuzia chini badala yake waweke bidhaa zao juu ya meza.

Akitembelea maeneo ya wafanyabiashara wa vyakula jana  Mjini Shinyanga, Mkuu huyo wa wilaya amesema vyakula kuwekwa chini ni hatari kwa afya za watumiaji wa vyakula hivyo kutokana na mazingira kutokuwa salama.

“Ni marufuku kuuza vyakula chini,tutamchukulia hatua yeyote tutakayemkuta akiuza vyakula zikiwemo mboga mboga chini”,amesema Mboneko wakati akitembelea eneo la Relini Ibinzamata mjini Shinyanga.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga, Jasinta Mboneko akiwaambia wafanyabiashara za vyakula wanaouza vyakula Relini Ibinzamata kando kando ya  Barabara kuu ya Tinde - Shinyanga kuondoa vyakula chini na kuweka kwenye meza - Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga, Jasinta Mboneko akiangalia vyakula vilivyowekwa chini ya ardhi.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga, Jasinta Mboneko akiangalia mihogo iliyowekwa chini.
Nani anauza  hivi vitungu.....
Mfanyabiashara ambaye siku chache zilizopita alikuwa anauzia bidhaa zake chini na kuamua kuanza kuuzia juu ya meza akifurahia baada ya Mkuu wa wilaya ya Shinyanga, Jasinta Mboneko kufika kwenye meza yake.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga, Jasinta Mboneko akiwapongeza wafanya biashara walioweka bidhaa zao juu ya meza.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga, Jasinta Mboneko akizungumza na wafanyabiashara walioweka bidhaa zao juu ya meza eneo la Relini Ibinzamata.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga, Jasinta Mboneko akiwashauri wafanyabiashara ya samaki kuondoka kando kando ya barabara.
Picha na Kadama Malunde - Malunde1 blog

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527