Breaking : HIACE YAGONGANA NA LORI NA KUUA WATU WANNE IKITEKETEA KWA MOTO BUKOBA


Watu wanne wamepoteza maisha katika ajali  iliyohusisha magari aina ya Canter lenye namba za usajili T223ATK na Hiace yenye namba za usajili T869 CHC kugongana  katika Mlima Nyangoye  eneo la Hamugembe Manispaa ya Bukoba mkoani Kagera.

Ajali hiyo imetokea usiku huu Februari 8,2019.

Kamanda wa polisi mkoa wa Kagera Revocatus Malimi,ambaye amefika eneo la ajali ambayo imetokea katikati ya barabara,amesema watu wanne wamefariki dunia katika ajali hiyo.

"Canter ilikuwa Main Road ikitokea Rwamishenye ikiingia Mjini kati,baada ya ajali hiyo kutokea,magari hayo yalitoka nje ya barabara,bahati mbaya gari aina ya Hiace ilishika moto na watu waliokuwemo waliungua moto,tumeondoa maiti mbili za abiria na dereva mwenye hiyo Hiace pia dereva wa bodaboda aliyekuwa amefunganishwa kwenye hii ajali bahati mbaya amefariki,kwa hiyo jumla ya watu waliofariki katika ajali hii ni watu wanne,mpaka sasa maiti zipo hospitali ya Mkoa hazijatambuliwa"- RPC

"Bado tunaendelea na shughuli ya uokoaji na uchunguzi kubaini hasa nini chanzo cha ajali hii na atakayebainika kusababisha ajali,hatua za kisheria zitachukuliwa",amesema Kamanda Malimi.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527