MAGUFULI AMTAKA WAZIRI ALIYEKAIDI AGIZO LAKE AJIANDAE KUACHIA OFISI

Rais John Pombe Magufuli amemtaka Waziri wa Madini, Dotto Biteko ajiandae kuachia ofisi yeye pamoja na Naibu Waziri wake endapo atashindwa kufunga kamera katika ukuta wa madini.

Rais amesema hayo leo wakati akihutubia mkutano wa Wachimbaji, Wafanyabiashara na Wadau wa sekta ya madini nchini.

"Niliagiza kufungwe Kamera katika ukuta wa Mererani lakini mpaka sasa hazijafungwa, ndio tatizo la Mawaziri wa Tanzania unatoa maagizo hawasikilizi" amesema Rais Magufuli.

Dkt. Magufuli ameongeza kwamba, "Nakuagiza tena Waziri Biteko, kafunge kamera ndani ya mwezi huu maana usipofanya hivyo ujiandae kuondoka na Naibu wako na makatibu wako, yaani hadi niondoke na nyie nimewamaliza".

Pamoja na hayo Rais ametaka Waziri Biteko kuwa mkali katika Wizara hiyo, "Nakuagiza uwe mkali, aliyekuwa Waziri mwenzako hakuwa mkali ndiyo maana nikaamua aende akapumzike ofisi ya Waziri Mkuu".

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post