WAKAZI WA WAZO NA VITONGOJI VYAKE WAPATA MAJI, WAZIRI PROF. MBARAWA AWAPA DAWASA KONGOLE


Waziri wa Maji na Umwagiliaji Prof. Makame Mbarawa (mwenye kofia) akishuhudia utokaji wa maji eneo la Kata ya Wazo mara baada ya kukamilika kwa tanki kubwa litakalowapatia maji kwa kipindi cha mwaka mzima bila kukatika.
Waziri wa Maji na Umwagiliaji Prof. Makame Mbarawa (mwenye kofia) akiongea na wananchi waliojitokeza kuchota maji.
Waziri wa Maji na Umwagiliaji Prof. Makame Mbarawa (mwenye kofia) akiongea na wananchi waliojitokeza kuchota maji huku akitoa maelekezo ya kuuza maji kwa tsh. 50 kwa ndoo.
Maji yakitoka.
Waziri wa Maji na Umwagiliaji Prof. Makame Mbarawa (mwenye kofia) akipata maelezo toka kwa Afisa Mtendaji Mkuu wa DAWASA Mhandisi Cyprian Luhemeja.

Na Cathbert Kajuna - Kajunason/MMG.

Mamlaka ya Majisafi na Majitaka Mkoa wa Dar es Salaam (DAWASA) imeanza kuwasambazia maji wananchi wa Kata ya Wazo na vitongoji vyake ikiwa ni utekelezaji wa ahadi iliyotoa jumapili Jan 13, 2019.

DAWASA imewekeza na imejenga tanki kubwa lenye uwezo wa kihifadhi lita milioni sita itakayofanya wakazi wa kupata maji kwa kipindi chote bila mgao.

Akizungumza na wananchi mara baada ya kumaliza kazi na kuwapatia wananchi maji, Waziri wa Maji na Umwagiliaji Prof. Makame Mbarawa amewaomba wasimamizi wa vizimba (Maduka ya kuuzia maji) kuuza maji kwa tsh. 50 kwa ndoo na si tsh. 100 kama ilivyokuwa awali.

"Leo mnafurahi kufunguliwa maji ila naomba muuze maji tsh. 50 kwa ndoo, sitaki kuona wananchi wanalalamika eti bei kubwa, mimi ndiyo msimamizi naomba mtekeleze mkumbuke na kulipa ankara zenu za maji ili DAWASA waweze kuwahudumia vyema," amesema.

Mwishoni kwa wiki iliyopita DAWASA kupitia Afisa Mtendaji Mkuu wa DAWASA Mhandisi Cyprian Luhemeja mbele ya wananchi akiwemo Mkuu wa Wilaya Kinondoni Daniel Chongolo, aliwaahidi wakazi wa kata ya Wazo na vitongoji vyake kuanzia wiki hii maji watapata bila mgawo wowote.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527