Picha : MKUU WA WILAYA YA SHINYANGA AGAWA VITAMBULISHO KWA WAFANYABIASHARA WADOGO... AWAKUMBUSHA NIDHAMU YA FEDHA

Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko amewakabidhi wafanyabiashara wadogo Vitambulisho Maalumu vilivyotolewa na Mheshimiwa Rais Dr John Pombe Magufuli huku akiwataka kuwa waaminifu na wazalendo wa taifa lao. 


Uzinduzi wa kutolewa vitambulisho hivyo umefanyika Alhamisi Januari 10,2019 katika ukumbi wa mikutano uliopo katika jengo la ofisi ya Mkuu Wilaya ya Shinyanga. 

Akizindua zoezi hilo Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko aliwataka wafanyabiashara hao kuwa na nidhamu katika matumizi ya fedha zinazopatikana kutokana na shughuli wanazofanya ili ziweze kuwanufaisha na kuwaondoa katika hali ya umaskini. 

“Tuwe na nidhamu ya matumizi ya fedha , umeshalipa kodi yako ya shilingi 20000 kwa mwaka mmoja utapewa kitambulisho na mwaka mwingine unatakiwa ulipe, sasa utakapolipa maana yake fedha utakazokuwa unaendesha biashara zisiingie tumboni tu zikafanye pia maendeleo kwenye familia yako” ,alisema Mboneko. 

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Manispaa ya Shinyanga Geofrey Mwangulumbi ametahadharisha Wafanyabiashara wakubwa kutojihusisha na udanganyifu kuuza bidhaa zao kwa kuwatumia wafanyabiashara ndogondogo wenye vitambulisho vilivyotolewa na Mheshimiwa Rais Magufuli kwani kwa kufanya hivyo ni kukwepa ulipaji wa kodi. 

“Unakuta mtu anaduka anatoa bidhaa za kwake anawapatia hawa wafanyabiashara ndogondogo ambao hawalipi kodi kwa hiyo anafunga duka lake wakati bidhaa zake zikiendelea kuuzwa mtaani, huyu anakwepa kulipa kodi na tumeshawabaini na tutawachukulia hatua” alisema Mwangulumbi. 

Kwa upande wao Wafanyabiashara ndogo ndogo wameshukuru na kupongeza hatua ya Mheshimiwa Rais Dr John Pombe Magufuli kutoa vitambulisho hivyo ambavyo vitawasaidia kufanya shughuli zao kwa amani na utulivu ikilinganishwa na hapo Mwanzo ambapo walikuwa wakipata usumbufu.

ANGALIA PICHA 

Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko akizungumza wakati akiwakabidhi wafanyabiashara wadogo Vitambulisho Maalumu vilivyotolewa na Mheshimiwa Rais Dr John Pombe Magufuli . Picha zote na Steve Kanyefu Malunde1 blog

Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko akiwataka wafanyabishara  kuwa waaminifu na wazalendo wa taifa lao 
Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko akikagua baadhi ya fomu ambazo mfanyabiasha ndogondogo anatakiwa kujaza taarifa zake ili apatiwe kitambulisho 

Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko  akiongoza zoezi la kuwapatia vitambulisho baadhi ya wafanyabiashara waliohudhuria katika uzinduzi wa utolewaji wa vitambulisho uliofanyika katika ukumbi wa mikutano uliopo katika jengo la ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga.
Mkurugenzi wa Manispaa ya Shinyanga Geofrey Mwangulumbi akisisitiza jambo ambapo amewataka wafanyabishara kuzingatia usafi katika mazingira ya biashara zao.

Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko (katikati),kushoto ni Mkurugenzi wa Manispaa ya Shinyanga Geofrey Mwangulumbi na kulia ni Meneja wa Mamlaka ya Mapato Tanzania TRA Mkoa wa Shinyanga Jumbe Samson wakisikiliza kwa makini baadhi ya maoni ya Wafanyabishara

Mkuu wa Wilaya akisisitiza jambo kwa baadhi ya wafanyabishara waliohudhuria katika uzuinduzi wa kugawa vitambulisho kwa wafanyabiashara ndogondogo

Meneja wa TRA Mkoa wa Shinyanga Jumbe Samson akiwasisitiza wafanyabishara kutumia vyema vitambulisho hivyo ili kuepuka usumbufu pindi ukaguzi wa kuwabaini wasio na vitambulisho utakapoanza.
Baadhi ya Wafanyabishara wakiwa ukumbini

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527