URAIS WA TUNDU LISSU WAMVURUGA MBUNGE MUSUKUMA CCM

Mbunge wa Geita Vijijini, Joseph Kasheku (Musukuma) amefunguka juu ya kauli ya Mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lissu kuwa akipewa nafasi ya kugombea Urais yuko tayari kukiwakilisha chama chake na kudai suala hilo lilikuwa ni ndoto yake.

Musukuma amedai kauli ya Tundu Lissu inaonesha alikuwa akitamani kuwania nafasi ya Urais kwa muda mrefu ndiyo maana amekuwa haonekani mara kwa mara kwenye jimbo lake bali anafanya siasa za kitaifa.

Musukuma amesema, "ukiona mtu aliyenusurika kufa halafu ameamka tu anawaza Urais maana yake alikuwa na ndoto ya kuwa rais wa Tanzania ndiyo maana alipotoka tu kwenye matibabu akasema anataka kuwa Rais wa nchi."

"Tumuombe Mungu kwa kuwa tu amelitanguliza suala la mapenzi ya jinsia moja hata huko kwenye chama chake naamini kuna watu hawataki ushoga kama tumekaa miaka yote bila kupitisha ushoga kwanini tupitishe ushoga kwenye Urais wa Tundu Lissu", ameongeza Musukuma.

Mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lissu kwa sasa yuko nchini Ubelgiji kwa ajili ya matibabu kufuatiwa kushambuliwa kwa risasi mwishoni mwa mwaka 2017 na hivi karibuni baada ya kupata nafuu alitangaza nia ya kuwania Urais endapo ataaminiwa na chama chake.

Pakua App mpya ya Malunde 1 blog imeboreshwa zaidi ili kukidhi mahitaji ya wasomaji wetu. Hii ndiyo mpya kabisa,ina alama hii ↡↡
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Ni rahisi sana : Ingia Play store kisha Andika Malunde 1 blog halafu bonyeza Install

https://bit.ly/2Qb7qyF


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527