STAND UNITED YAGUBIKWA NA MATUMIZI MAKUBWA KULIKO MAPATO

Timu ya Stand United maarufu kwa jina la chama la wana inayofadhiliwa baadhi ya huduma na kampuni ya vinywaji ya Jambo products,imeelezwa kukabiliwa na changamoto ya kuwa na matumizi makubwa tofauti na mapato hali inayoisababisha timu hiyo kujikongoja kwenye michuano ya ligi kuu soka Tanzania bara. 


Timu hiyo imecheza michezo 20 na kupata alama 22 ikiwa nafasi ya 11 kati ya timu 20 zinazoshiriki ligi kuu soka Tanzania bara. 

Mwenyekiti wa timu hiyo Dkt. Ellyson Maeja alisema timu hiyo katika mzunguko wa kwanza msimu huu wamepata fedha kutoka wadhamini mbalimbali jumla ya kiasi cha shilingi milioni 53.6 (Azam milioni 27,BIKO milioni 13,viingilio mechi za nyumbani milioni 3.6). 

Maeja aliongeza kwamba bajeti ya mishara ya wachezaji na benchi la ufundi imekuwa ikishuka kila wakati na hali inayowanja moyo. 

“Bajeti ya mishahara mwezi Agosti 2018 ilikuwa milioni 16.3 kwa mwezi,lakini imeshuka kufikia milioni 14, na tunaendelea kushusha ingawaje kubana mkaa sana napo ni shida”, Alisema Maeja. 

Kampuni ya vinywaji ya Jambo Products inaifadhili timu hiyo huduma ya usafiri ndani na nje ya mkoa, chakula pindi timu inapokuwa ndani ya mkoa wa Shinyanga,  huduma ya maji ya kunywa na jezi za wachezaji. 

Wadau wa soka mkoai Shinyanga wamemuomba mfadhili huyo kufadhili mambo ambayo ni changamoto kwa timu hiyo kama vile fedha ya mishahara pamoja na usajili kwa wachezaji. 

Wadau hao wa soka wanakutana Januari 10 2019 kujadili na kuweka mikakati ya kuinusuru timu hiyo na hali mbaya ya kiuchumi na kuleta ushindani katika ligi kuu soka Tanzania bara nakuendlea kuwanufaisha wakazi wa mkoa wa Shinyanga kiuchumi. 

Na Malaki Philipo - Malunde1 blog


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post